May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Trump alivyowaaga Wamarekani

Donald Trump, Rais wa Marekani anayemaliza muda wake

Spread the love

DONALD Trump, ametoa hotuba yake ya mwisho akiwa Rais wa Marekani akisema, “Tumefanya kile ambacho tulikuja kukifanya na tumefanya mambo mengine mengi.” Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Trump anahitimisha utawala wake wa miaka minne leo Jumatano tarehe 20 Janauri 2021, na kumpisha Joe Biden wa Demokrati kuongoza Taifa hilo kubwa duniani.

Biden mwenye miaka 78, atakuwa rais wa 46 wa Marekani mwenye umri mkubwa zaidi katika historia ya taifa hilo.

Katika video aliyoiweka kwenye mtandao wa YouTube, Rais Trump amesema “mapambano yalikuwa makali, vita ilikuwa ngumu, kwasababu hicho ndicho mlinichagua kukifanya.”

Trump anayekiwakilisha chama cha Republican, ataondoka madarakani akiwa hakubaliani na matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Novemba 2020, ambayo yamempa ushindi Joe Biden na makamu wake, Kamala Harris.

Joe Biden, Rais Mteule wa Marekani

Utawala wa Trump, umekuwa ukikumbwa na ghasia za hapa na pale na tarehe 6 Januari 2021, wafuasi wake, walivamia jengo la Bunge la Capitol Hill, wakipinga matokeo ya uchaguzi, wakati Bunge hilo lilipokutana kuidhinisha matokeo ya uchaguzi.

“Ghasia za kisiasa ni shambulio la kila kitu tunachothamini kama Wamarekani. Kamwe hatuwezi kuvumilia,” amesema Trump huku akishindwa kutambua matokeo yaliyompa ushindi Joe Biden

Katika hotiba ya Trump, ya dakika 20, amesema utawala wake umefanya kile ambacho walikuja kukifanya na wamefanya zaidi.

“Vita ilikuwa kubwa, mapambano yalikuwa makali, ni maamuzi magumu kwasababu hiyo ndio sababu iliyowafanya mnichague,” amesema.

Kamala Harris, Makamu wa Rais wa Marekani

Biden ataapishwa mbele ya Jaji Mkuu wa Marekani, John Roberts, mjini Washington.

Sherehe za kuapishwa kwake, zitahudhuriwa na idadi ndogo ya watu na haitakuwa na shamrashamra kama za watangulizi wake kufuatia janga la maambukizo ya viruso vya corona (COVID-19).

Pia, kutokana na hofu za kiusalama baada ya kisa cha wafuasi wa Rais Trump kuvamia majengo ya Bunge Capitol Hill mjini Washington tarehe 6 Januari 2021, hali iliyofanya ulinzi kuimalizwa zaidi.

error: Content is protected !!