May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yapitisha vigogo 5 baraza la wadhamini

Mama Fatma Karume, Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Yanga

Spread the love

 

MKUTANO Mkutano Mkuu wa Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, imepitisha majina matano likiwemo Mama Fatuma Karume, kuwa wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa timu hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Majina hayo, yamepitishwa leo Jumapili, tarehe 27 Juni 2021, katika mkutano mkuu huo wenye lengo la kufanya mabadiliko ya katiba ili kuifanya kuendeshwa kisasa.

Kabla ya kupitishwa, Mweneykiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla ameyatangaza mbele ya wajumbe majina hayo likiwemo la Mama Fatma ambaye ni mjane wa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Aman Karume.

George Mkuchika

Wengine ni; mawaziri wa serikali ya Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba wa Fedha na Mipango na Kepteni mstaafu George Mkuchika, Waziri Ofisi ya Rais-Kazi Maalum.

Pia, wamo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji, Geofrey Mwambe na Mbunge wa Kinondoni (CCM), Abbas Tarimba.

Abbas Tarimba

Wajumbe hao watano, watamchagua mwenyekiti pindi watakapokutana.

error: Content is protected !!