May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TRA yaaanza mchakato somo la kodi lifundishwe shuleni

Alphayo Kidata, Kamishna Mkuu wa TRA

Spread the love

 

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wanafanya mazungumzo ya kuwezesha somo la ulipaji kodi lianze kufundishwa shule za awali na msingi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata, wakati akitoa mrejesho wa mamlaka yake kwenye kongamano la siku 100 za utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan, zilizotimia leo Jumapili, tarehe 27 Juni 2021.

Kongamano hilo, linatoa mrejesho kwa wadau wa Baraza la Wafanyabiashara (TNBC), ambalo limefanyika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam na kufunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

“Ni wajibu kila mmoja wetu kuwa na wajibu kama unatakiwa kulipa kodi unalipa bila kusukumwa ili kuwezesha kuijenga nchi yetu.”

“Tunashirikiana na wizara ya elimu ili somo la kodi lianzie kufundishwa kuanzisha shule ya msingi na awali ili wajue umuhimu wa kulipa kodi,” amesema Kidata.

Kidata amesema, katika kipindi cha miezi miwili, wamefanikiwa kurejesha Sh.92 bilioni za marejesho ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kati ya Sh.844 bilioni wanazodaiwa na wafanyabiashara.

Amesema, awali madeni hayo yalikuwa yakihakikiwa na TRA kwa asilimia 100, lakini kuanzia tarehe 1 Julai 2021, itakapoanza bajeti mpya ya serikali 2021/22, uhakiki huo hautakuwa ukifanywa na mamlaka hiyo kwa mujibu wa sheria ya fedha ya 2021.

Kidata amesema, walikuwa wanadaiwa Sh.57 bilioni za dhamana ya sukari ya viwandani, lakini baada ya uhakiki Sh.8 bilioni hazikukidhi mahitaji na mpaka sasa wamelipa zaidi ya Sh.35 bilioni.

error: Content is protected !!