October 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yaitisha mkutano wa dharura kubadili Katiba

Jengo la Yanga

Spread the love

MWENYEKITI wa Yanga. Dk. Mshindo Msola ameitisha mkutano mkuu wa dharura kwa wanachama wa klabu hiyo unaotarajia kufanyika tarehe 16 Februari, 2020, katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwl. Nyerere. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mkutano huo ambao utakuwa na agenda kuu sita zikiwamo kuwasilisha na kuainisha mapendekezo ya katiba ya sasa na mapendekezo mapya na wanachama kupigia kura marekebisho ya katiba.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo imeeleza kuwa Mwenyekiti ameitisha mkutano huo wa dharura kwa mujibu wa ibara ya 22 ya katika ya Yanga 2010.

Mabadiliko hayo ya katiba huenda yakaifanya klabu hiyo kutaka kuingia kwenye mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji kwa kutumia mgumo wa hisa kama alivyo nukuliwa mwenyekiti wa klabu hiyo siku za nyuma kusema kuwa mpaka kufikia mwezi wa tano klabu hiyo itaingia katika mchakato wa mfumo wa mabadiliko.

error: Content is protected !!