April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mahabusu wabebwa kwa bodaboda

Spread the love

UKOSEFU wa usafiri katika Gereza la Ulanga, Morogoro, imesababisha mahabusu kusafirishwa kwa bodaboda kupelekwa mahakamani. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 28 Januari 2020, na Goodluck Mlinga, Mbunge wa Ulanga (CCM) wakati akiihoji serikali kwamba ina mkakati gani kuepuka utaratibu huo?

Mbunge huyo pia amehoji, ni lini serikali itapeleka gari katika gereza hilo ili kueuka usumbufu huo?

Akijibu swali hilo, Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani amesema, changamoto hiyo itatatuliwa kadri itakavyowezekana.

Hata hivyo, Job Ndugai, Spika wa Bunge ameonesha kushangazwa na hatua hiyo, huku akisema “hii nayo mpya…”

error: Content is protected !!