May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga na Mwadui, Simba na Dodoma Jiji, robo fainali Kombe la Shirikisho

Spread the love

RATIBA ya michuano ya Kombe la Azam Federation CUP (ASFC) nchini Tanzania, hatua ya robo fainali, itashuhudia Yanga ikisafiri kwenda Shinyanga kuwavaa Mwadui FC. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Wakati Yanga ikisafiri, watani zao Simba, mabingwa watetezi wa michuano hiyo, itakuwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, kuwaalika Dodoma Jiji.

Ratiba hiyo, imepangwa leo Jumanne, tarehe 11 Mei 2021, huku timu zingine kwenye hatua hiyo ya robo fainali ni Biashara United itatumia uwanja wake wa Karume, Mkoa wa Mara kuwaalika Namungo FC ya mkoani Lindi.

Rhino Rangers yenyewe itavaana na Azam FC. Michezo hiyo ya robo fainali, itachezwa kati ya tarehe 25 hadi 27 Mei 2021.

Mshindi kati ya Simba dhidi ya Dodoma Jiji, atavaana na mshindi kati ya Rhino Rangers dhidi ya Azam FC huku Biashara United dhidi ya Namungo watacheza na mshindi kati ya Mwadui FC dhidi ya Yanga.

error: Content is protected !!