May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bilioni 9.8 kujenga Hospitali ya Rufaa mkoa wa Katavi

Ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Katavi

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imetenga kiasi cha Sh. 57 bilioni kwa ajili ya ukamilishaji wa miundombinu ya hospitali za rufaa za mikoa ukiwemo mkoa wa Katavi ambao zimetengwa Sh. 9.8. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea)

Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne, tarehe 11 Mei, 2021, bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Godwin Mollel, alipokuwa akijibu swali la Sebastian Kapufi, Mbunge wa Mpanda Mjini.

“Je, ni lini serikali itamaliza ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Katavi, kwani ujenzi huo unakwenda kwa kusuasua?” ameuliza Kapufi.

Dk. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Mollel amejibu, wizara inaendelea na ujenzi wa hospitali ya Mkoa wa Katavi ambapo kwa sasa ujenzi umekamilika kwa wastani wa asilimia 70.

Amesema, ujenzi huo kwa upande wa maabara umefikia asilimia 98, na jengo kuu la hospitali umefikia asilimia 42.

“Mradi huu unagharimu jumla ya Sh. 9.82 bilioni, ambapo hadi sasa kiasi cha Sh.3.97 kimetolewa na kutumika.

“Katika mwaka wa fedha 2021/22, serikali imetenga kiasi cha Sh. 57 bilioni kwa ajili ya ukamilishaji wa miundombinu ya hospitali za rufaa za mikoa,” amesema Mollel.

Mollel amesema, aidha serikali imetenga kiasi kilichobaki cha Sh.5.85 ambazo zitatumika kukamilisha ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Katavi ifikapo Januari 2022.

error: Content is protected !!