September 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Yanga mguu sawa kuikabili Kagera

Spread the love

USHINDI wa mabao 3-2 dhidi ya Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kikosi cha Yanga kimejiimalisha kuikabili Kagera Sugar, katika mchezo wa kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Yanga wanatarajia kuikabili Kagera Sugar,  tarehe 30 Juni, 2020 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam katika harakati ya kutafuta tiketi ya kufuzu nusu fainali ya kombe hilo.

Mabao ya Yanga kwenye mchezo wa leo yamefungwa na Deusi Kaseke (6, 45+2) na baadae kufuatia na bao la ushindi la Mrisho Ngassa (73) aliyeingia kuchukua nafasi ya Ditram Nchimbi.

Kwa upande wa Ndanda FC,  mabao yao yalipachikwa na Abdul Hamis (10) na dakika tano baadae Vitaris Mayanga akaandika bao la Pili kwa mpira wa adhabu ndogo.

Kwa matokeo hayo Yanga inajisogeza mpaka nafasi ya pili baada ya kufikisha pointi 59, ikiwa tofauti ya pointi moja na Azam Fc ambao wamelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Biashara.

error: Content is protected !!