October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba bado mbili, Yanga yaishusha Azam FC

Wachezaji wa timu ya Azam wakiwa katika moja ya michezo yake ya Ligi Kuu Tanzania Bara

Spread the love

MICHEZO nane imechezwa leo kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo klabu ya Yanga imefanikiwa kuishusha Azam FC kwenye msimamo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Ndanda, huku Azam FC wakisubilisha Simba ubingwa baada ya kwenda sare ya bao 1-1 dhidi ya Biashara United. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa matokeo hayo ya Azam FC dhidi ya Biashara yatailazimu Simba kushinda kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Tanzania Prisons ili waweze kutangaza ubingwa.

Mtibwa Sugar ameendelea kupata wakati mgumu baada ya kukubalia kipigo cha bao 1-0, dhidi ya Mwadui huku Namungo akilazimishwa sare ya bao 1-1, dhidi ya Ruvu Shooting.

Matokeo mengine ya michezo ya leo Alliance imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union, Singida amekubali kichapo cha mabao 3-2 akiwa nyumbani mbele ya Lipuli Fc.

KMC wamelazimishwa sare ya bao 1-1 na Kagera Sugar kwenye Dimba la Kaitaba na Mbeya City ameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Jkt Tanzania.

error: Content is protected !!