September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba washindwe wao tu, mashabiki waruhusiwa kusherekea ubingwa

Spread the love

SERIKALI kupitia Baraza la Michezo Tanzania (BMT), imeruhusu mashabiki kuingia uwanjani katika mchezo kati ya Tanzania Prisons na Simba utakaochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine siku ya Kesho. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Ni siku chache tu zimepita toka Serikali kuzuia mashabiki kwenye michezo ya Ligi Kuu kwa klabu zinazocheza dhidi ya Simba na Yanga kwenye viwanja vyao vya nyumbani kutokana na kutofuata muongozo uliotolewa na Wizara ya Afya.

Katika taarifa hiyo serikali imesema kuwa ilipata maombi kutoka kwa ofisi ya afisa Tarafa mkoa wa Mbeya ya kuruhusu mashabiki kuingia kwenye mchezo wa kesho kutokana na kujipanga kuthibiti vizuri mkusanyiko ikiwa sambamba na kuingiza mashabiki wachache.

Mchezo huo ambao utakuwa muhimu kwa upande wa Simba kutokana na nafasi kubwa waliyonayo ya kutangaza ubingwa kama wakifanikiwa kuibuka na ushindi.

Aidha serikali imeeleza kuwa kama wahusika wa uwanja huo watashindwa kusimamia vizuri taratibu hizo, huenda wakachukuliwa hatua kali ikiwamo kuufungia Uwanja kutotumika kwenye michezo yoyote ya Ligi Kuu.

Ikumbukwe mchezo wa mzungo wa kwanza uliokutanisha timu hizo kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es Salaam ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.

error: Content is protected !!