December 4, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri wa JK afariki dunia

Spread the love

OMARY Nundu, aliyewahi kuwa Mbunge wa Tanga Mjini na Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete, amefariki dunia leo tarehe 11 Septemba 2019. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Taarifa ya kifo chake imetolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kitengo cha mawasiliano kwamba waziri huyo wa zamani, alifikishwa kwenye hospitali hiyo akiwa amefariki.

“Waziri wa zamani Mh.Omary Nundu alifikishwa leo MNH ,akitokea nyumbani kwa gari binafsi la wagonjwa akiwa tayari ameshafariki ,hivyo waliomleta waliamua wakahifadhi mwili wake katika Hospitali ya Rufaa ya Jeshi Lugalo,” imeeleza taarifa hiyo.

Nundu amefariki akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania baada ya kuteuliwa na Rais John Magufuli kushika nafasi hiyo tarehe 12 Juni 2019.

error: Content is protected !!