October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wilaya 27 hazina mahakama za wilaya-Dk. Mahiga

Spread the love

SERIKALI imesema, ni kweli Wilaya ya Itilima kwa sasa haina Mahakama ya Wilaya, hivyo wananchi wanalazimika kusafiri kwa umbali wa kilometa 37 kufuata huduma katika Wilaya ya Bariadi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Hayo yameelezwa leo tarehe 11 Agosti 2019 bungeni na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Augustine Mahiga, alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Gimbi Masaba (Chadema).

Katika swali na msingi la mbunge huyo, alitaka kujua ni lini serikali itajenga mahakama ya wilaya katika Wilaya ya Itilima?

Dk. Mahiga akijibu swali la msingi amesema, ni kweli wilaya hiyo haina Mahakama ya Wilaya na wananchi wanalazimika kusafiri kwa umbali wa kilometa 37 kufuata huduma katika wilaya ya Bariadi.

Aidha, amesema kuwa changamoto hiyo ipo katika wilaya 27 nchini ambazo zinapata huduma katika wilaya za jirani, na hali hiyo inatokana na ukweli kwamba Mahakama ya Tanzania bado inakabiliwa na uhaba wa majengo katika maeneo mengi.

“Kama ambavyo nimekuwa nikieleza katika bunge lako tukufu, mahakama imejiwekea mkakati wa kutatua changamoto hii, hatua kwa hatua kupitia mpango wake na miaka mitano ya kujenga na kukarabati majengo ya mahakama kwa ngazi zote.

“Mahakama ya Wilaya ya Itilima ipo katika mpango wa kujengwa katika mwaka wa fedha 2019/20 pamoja na mahakama nyingine katia wilaya ya Busega, Kyerwa, Misenyi, Gairo, Mbogwe, Songwe,Nyang’wale,Mvomero pamoja na wilaya nyingine zenye uhitaji” ameeleza Dk. Mahiga.

Aidha amesema, anashukuru uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Itilima kwa kutoa kiwanja cha kujenga mahakama ya wilaya, chenye ukubwa za mita za mraba 5,028.

error: Content is protected !!