April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wakili wa Mbowe, shahidi Jamhuri walivyotoana jasho 

Spread the love

BERNALD Nyambari, aliyekuwa Msaidizi wa Upepeli Mkoa wa Kipolisi Kinondoni na shahidi namba nane wa Jamhuri katika kesi ya uchochezi namba 112/2018, inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake wanane, amehojiwa unadhifu wake? Anaripoti Faki Ssosi…(endelea).

Wakili wa utetezi Peter Kibatala, leo tarehe 11 Agosti 2019 amemhoji Nyambari “kwanini hukuvaa vesti?” ili aonekane nadhifu mahakamani.

Ilikuwa ni awamu ya pili ya maswali baada ya mapumziko kwenye kesi hiyo inayowahusu Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu-Taifa; John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu – Bara na Salumu Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu -Z’Bar.

Wengine ni Ester Matiko Mbunge wa Tarime Mjini; Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini na Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini.

Mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo;-

Kibatala: Ni sahihi kuwa ofisa wa polisi lazima awe nadhifu?

Shahidi: Polisi lazima awe nadhifu

Kibatala: Mwambie hakimu kwanini hujavaa vesti?

Shahidi: Sifahamu kifungu chochote kinachosema nikivaa nguo za kirai lazima nivae vesti

Kibatala: kwanini hukuvaa vesti?

Shahidi: Ni utashi wangi

Kibatala: Kwanini hujachomekea?

Shahidi: Sipendelee kufanya hivyo

Kibatala: haya…. Nimekusikia sahihi kwamba Akwelina alipigwa risasi?

Shahidi: taarifa nilizonazo alikufa kwa kupigwa risasi

Kibatala: Ni Sahihi kwa taarifa ulizonazo wewe Akwelina alipigwa risasi kwenye tukio linalohusisha washtakiwa

Shahidi: Ni sahihi kwamba alipigwa risasa kwenye tukio hilo

Kibatala: Ni sahihi kwamba bint huyo Mungu amrehemu, alipiga risasi akiwa anaelekea kwenye shughuli zake?

Shahidi: Nilieleza alikuwa kwenye shughuli zake

Kibatala: Ni sahihi kwamba wale waandamanaji walikuwa na mawe, fimbo pamoja na chupa za maji tu?

Shahidi: Vifaa vinavyoneka

Kibatala: vifaa ulivyovitja

Shahidi: ndio vifaa vilivyokuwa vinaonekana

Kibatala: Wakati unaongozw na Wakili wa Serikali uliongozwa kusema waandamanaji walikuwa na bunduki

Shahidi: Sikuongozwa

Kibatala: Ulifanya zoezi la utambuzi uliwatambua watu wafuatao ni Mbowe, Mashinji, Mdee na Mnyika Spefical kama ulisema lolote juu ya kuwa walikuwa na bunduki?

Shahidi: Sikusema

Kibatala: mwambie hakimu husema chochote juu ya kupatika kwa bunduki au bastola eneo la tukio

Shahidi: Hakuna bunduki au bastola iliyopatika

Kibatala: Katika Upelelezi wako ulisema ulifanya uchunguzi wa kuona, mwambie hakimu kama uliokota maganda ya risasi eneo ambalo ulisema umeokota chupa

Shahidi: Sikusema chochote kuhusiana na maganda ya risasi

Kibatala: Ni Sahihi mawe, chupa za maji ma vifaa vilivyoachwa kwene eneo la tukio

Shahidi: ndio

Kibatala: Mwambie hakimu kama uliongozwa kusema chochote juu ya ukaguzi silaha wanazomiliki kihalali waandamani mmoja au wengi

Shahidi: Sikusema chochote

Kibatala: Shahidi je, kati ya wale uliwataka Mbowe, Mdee, Mashinji na Mnyika uliongozwa kuhusiana na kukagua Silaha zao kwamba kuna mmoja alifyetua?

Shahidi: Sikusema chochote

Kibatala: Unafahamu au hufahamu hao washtakiwa wanamiliki silaha?

Shahidi: Nafahamu Mbowe anamiliki Silaha

Kibatala: aina gani

Shahidi: Belleta

Kibatala: hujaifanyia ukaguz?

Shahidi: Sijaifanyia

Kibatala: Unafahamu kama Mbowe alikuwa na hiyo silaha wakati wa tukio?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Eneo la tukio kulikuwa na Polisi wenye silaha wangapi?

Shahidi: wengi kama watano

Kibatala: aina gani?

Shahidi: SMG

Kibatala: Uliongozwa kusema chochote juu ya hizo silaha tano kuzikagua pengine zilimpiga Akwelina?

Shahidi: Sikuongozwa

Kibatala: Alipigwa risasi eneo gani huyo marehemu?

Shahidi: Alipigwa risasi kichwani

Kibatala: alipigwa kwa umbali au ukaribu?

Shahidi: siwezi kujua

Kibatala: uliongozwa kusema chochote kuhusiana na majerani waliokaa karibu kwenye daladala na Akwelina waliongea chochote kwenye upelelezi wako?

Shahidi: sikuongozwa

Kibatala: Uliongozwa kusema chochote juu ya maofisa wa polisi kuhusishwa na kumpiga risasi Akwelina?

Shahidi: Sikuongozwa

Kibatala: Wewe ni mwanasheria maana ya maneno ya kuambiwa unafahamu?

Shahidi: ndio

Kibatala: Nikisema ni umbea nitakuwa sahihi?

Shahidi: sio sahihi ni maneno ya kusikia kwa watu wengine

Kibatala: wewe binafsi uliwasikia washtakiwa kwenye viwanja vya buibui wakitoa maneno ya uchochezi?

Shahidi: sikuwepo

Kibatala: wewe binafsi uliwasikia wakitoa maneno ya kujaza chuki?

Shahidi: sikuwasikia moja moja kwa moja kwa sababu

Hakimu: hiyo sababu iache

Kibatala: Wakati unaongozwa jana na leo Dada yangu alikonesha hati ya mashtaka na kuongozwa maneno hayo wameyasema huyo na huyo

Shahidi: sikuongozwa

Kibatala: Hapo awali uliwataja ni nani na nani alikuwepo kwenye viwanja vya Buibui?

Shahidi: unataka niseme nani na nani au?

Kibatala: Hapo awali uliwataja ni nani na nani alikuwepo kwenye viwanja vya Buibui?

Shahidi: Niliwataja kwa jumla kama sikutaja huyo alikuwa Buibui au Mkwajuni kama unataka niende spesific

Kibatala: Ulisema kwamba moja ya vyanzo vyako ni Bloggs.

Hakimu Simba aliahirisha kesi kuanzia saa 6 na nusu hadi saa saba na kisha Wakili Kibatala aliendelea

Kibatala: Shahidi ni sahihi maneno uliyodai yametamkwa uliyasikia kwenye Bloggs?

Shahidi: Ni pamoja na kwenye Bloggs na kupitoa recods zilizofanywa kwenye mikutano

Kibatala: Mwambie mheshimiwa hakimu iwapo kuna Blogg iliitaja?

Shahidi: Hakuna Blogg niliyoitaja

Kibatala: Shahidi unafahamu kwamba Blogg ili iitwe Blogg kisheria lazima ipitie taratibu fulani za kisheria pale TCRA?

Shahidi: Nafahamu lazima isaijiliwe TCRA

Kibatala: Sasa Shahidi unafahamu Usajili uniafanya Blogg kuwa Safy kwenye mikono ya TCRA?

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Kwa ushahidi wako wewe moja ya ushahidi wako ni Blog tuashumu Blog hiyo imesajili swali langu pamoja na hayo yote uliongozwa kusema kuwa maneno niliyoyasikia ni haya hata kama sio neno kwa neno lakini ni maudhii

Shahidi: Sikuongozwa

Kibatala: Ndio maana nakueleza hear say ni umbea… katika hizo rekodi uliwahi kuona maandamano yakioneshwa waandamanaji wakiwa kwenye Bararaba ya Kawawa

Kibatala: Mwambie hakimu uliona mwaka gani?

Shahidi: Tarehe 18 Februali kupitia Muungwana Blogg

Kibatala: Uliwahi kuzungumza na mtu wa Muungwana Blogg?

Shahidi: Nilizungumza na Mwandishi anaitwa Charles

Kibatala: Ni ushahidi wako kwamba Charles ndiye aliyepiga picha yeye binafsi na kuziweka Muungwana Blog?

Shahidi: ndoo

Kibatala: Je kuna mtu mwengine aliyepiga picha zaidi ya Charles?

Shahidi: Hakuna mtu mwengine

Kibatala: Uliongea na Charles baada ya kuona Muungwana Blog au kabla?

Shahidi: Niliongea baada ya kuona

Kibatala: Unamjua mkurugenzi wake?

Shahidi: Mkurugenzi Ofisi namjua mtu mmoja anaitw Rashid

Kibatala: Ni muasia au mweusi?

Shahidi: anaonekana kama mwarabu

Kibatala: Twende kwenye Contet (maudhui) ya kile ulichokiona, mwambie hakimu kama ulioneshwa contet zile angalau kuzitambua ili uzitambue

Shahidi: hapana

Kibatala: Shahidi ukitoa uliyoiona Muungwana Blog uliwahi kuona video iliyopigwa na Ofisa wa Polisi anayefanya kazi Ofisi ya RCO?

Shahidi: Sijawahi kuona.

Kibatala: Uliwahi kuongea na Ofisa yoyote wa Polisi kama mpelelezi aliyepiga picha hizo?

Shahidi: Niliongea naye

Kibatala: Anaitwa nani?

Shahidi: Charles

Kibatala: Ulimuhojia tarehe ngapi mwezi gani?

Shahidi: baada ya kutokea tukio hilo

Kibatala: kwa ushahidi wako kama mpelelezi ulimuhoji shahidi bila kuona kile alichokwenda kufanya

Shahidi: Nimhoji yeye kama shahidi na juu ya alichofanya kwenye alichopiga picha

Kibatala: Shahidi Twende pale Kawawa ulipofika ulikuta mabom shapigwa ua yalishapigwa

Shahidi: nilikuwata mabom yanaanza kupigwa

Kibatala: Ni Ushahidi wako wakati linatolewa tangazo la ILANI ulikuwepo

Shahidi: Sikuwepo

Kibatala: Tusaidie kazi ya ILANI nini kisheria

Shahidi: Ni kuwatawanya watu waliokusanyika kinyume cha sheria

Kibatala: Kuna kosa linafanyika kama ILani imetolewa na watu wamekusanyika

Shahidi: ni sahihi.

Kibatala: Shahidi kubishana na askari kabla ya Ilani ni kosa

Shahidi: sijasema kama watu walibishana na Askari

Kibatala: mheshimiwa naomba jibu lake liingie hivyo hiyo. Wewe ulitokea upande gani wa Moroko wa Magomeni?

Shahidi: Nilitoka eneo la tukio upande mwengine wa barabara

Hakimu: Ulitokea wapi?

Shahidi: ngoja nielezee ukiwa unatoka moroko unakwenda magomeni ukipata kituo cha basi cha Mkwajuni eneo la Hananasof lipo upande wa kushoto kama unatoka Moroko kwenda magomeni?

Kibatala: Kama nakuelewa vizuri kuna barabara ya tatu eneo la mkujuni

Shahidi: Kina Feeder road

Kibatala: ukitokea huko waandamanaji uliwapita au uliwaface

Shahidi: Niliwapita niliacha gari niliingia kwa mguu

Kibatala: Nichoree picha wakati mabomu yanapigwa ulikuwa upo kwenye kundi la Polisi au hujawafikia Polisi

Shahidi: Nilikuwa nawakaribia Polisi

Kibatala: mabomu yalipopigwa watu walitawanyika au hakutawanyika?

Shahidi: baadhi walitawanyika

Kibatala: Ni sahihi ulikuwa na askari wawili wanakusindikiza

Shahidi: sahihi

Kibatala: na Ulisema watu walikuwa wanamawe fimbo na wanaimba kisharishari

Shahidi: sahihi

Kibatala: hawa askari walikuwa wamevaa sare au kirai

Shahidi: kiraia

Kibatala: Hivi ukiwa umevaa kirai unaruhusiwa kumkamata mtu?

Shahidi: Unaruhusiwa kumkamata.

Kibatala: Shahidi wale waandamanaji wale waandamanaji walikuwa wameshika chupa walikuwa wamefanya kosa la jinai au hawakufanya kosa la jinai?

Shahidi: Walifanya kosa la jinai

Kibatala: Naomba umwambie Hakimu iwapo mulimkamata mwandamanaji mmoja au wawili

Shahidi: hatukumkamata mwandamanaji yoyote.

Kibatala: Baada ya mabom kupigwa ulikama waandamanaji au hamkumata

Shahidi: Ulikuwa unamaanisha sisi tuliovaa kiraia au wengine

Kibatala: nimekuuliza spesifical nyie watatu kuna mtu yoyote muliyemkamata

Shahidi: hakuna

Kibatala: Mulimshuhudia askari yoyote anamkamata mtu ambaye amekamatwa na chupa au fimbo

Shahidi: Nimeshuhudia

Kibatala: Swali langu lina sehemu mbili : mwambie hakimu ukitoa hawa watuhumiwa ulisema kulikuwa na waandamanaji 550 je unawafahamu wengine waliokamatwa?

Shahidi: Siwafahamu kwa majina

Kibatala: Hawa waandamanaji unafahamu walikuwa wa kundi gani Yanga, Simba , CCM au CUF?

Shahidi: Siwafahamu

Kibatala: Kabla ya siku ya tukio ulishawahi kupita Hananasif kutoka Mkwajuni

Shahidi: Nishawahi kupita

Kibatala: Ilikuwa shughuli za kipelelezi au Shughuli binafsi

Shahidi: Shughuli binafsi

Kibatala: Uliongozwa na mawakili wa Serikali kutofautisha wingi wa watu na matukio na shughuli

Shahidi: Sikuongozwa

Kibatala: Shahidi katika hawa watu uliowahoji uliongozwa kusema kuwa ulimuhoji Dereva wa Mwendo kasi?

Shahidi: Sikuongozwa

Kibatala: Uliongozwa kufafanunua kama ulimuhoji dereva wa Dalala akawa blocked na waandamanaji

Shahidi: Sikuongozwa

Kibatala: Uliongozwa kufafanunua kuhusu dereva yoyote aliyekuwa akipita hiyo nji

Shahidi: sikuongozwa

Kibatala: Madereva wa Amburance mulisema walikuwa blocked uliongozwa kusema chochote kuhusiana na kumhoji aidha eneo la tukio au kwenda kwenye hospitali ya Mwananyamala sambamba na namba za Amburance?

Shahidi: Sikuongozwa

Kibatala: Uliongozwa kusema chochote kuhusu kuwahoji hawa wamiliki wa hizi meza zilizopinduliwa?

Shahidi: Sikuongozwa

Kibatala: Uliongozwa kusema chochote juu ya Abiria wa mwendekosa aliyekwama kituo kutokana na athari za maandamano

Shahidi: Sikuongozwa

Kibatala: Ulisema kuwa baada ya tukio ulifanya zoezi la kuhoji watu ni sahihi

Shahidi: Niliwahoji

Kibatala: Ulianisha hawa watu uliowataja kwa majina kwamba maduka yao yalifungwa katika ushahidi wako ulianisha migahawa na maduka yaliyofungwa

Shahidi: Sikufanya hilo zoezi

Kibatala: hawa washtakiwa wanne walikamatwa kwenye tukio

Shahidi: hawakukamatwa

Kibatala: ulisema kulikuwa na askari wangapi kadiria kama ulivyokadiria wingi wa watu

Shahidi: kama askari 15

Kibatala: hawa Koplo Rahimu na Mwenzake uliwakuta eneo la tukio

Shahidi: sikuwakuta

Kibatala: Nani aliyekuambia hawa kina Koplo Rahimu aliumia ni kwa ufahamu wako au kuna mtu alikuambia

Shahidi: Niliambiwa na Ofisa Operesheni

Kibatala: Tuwazungumzie Koplo Rahimu na mwenzake PC Fikiri uliongozwa kitaja Hospitali ambayo uliwahoji?

Shahidi: Sikutaja

Kibatala: Uliongozwa kusema namna taratibu za kitabibu kwa watu majeruhi walivyokupokea na Ofisa tabibu yupi?

Shahidi: Sikuongozwa

Kibatala: Uliongozwa angalau kutaja tarehe uliyowahoji hawa maofisa wawili?

Shahidi: Sikuongozwa

Kibatala: Rahimu na Fikiri walipokuwa Hospital vitanda vyao vilikuwa umbali gani kuanzia hapo ulipo

Shahidi: kama hapa na hapa (akiwa kizimbani alipokaa kama hatua tano )

Kibatala: kama hatua tano

Shahidi: ndio

Kibatala: walikuwa wodi moja

Shahidi: ndio

Kibatala: Tarehe ngapi uliwahoji

Shahidi: tarehe 17 Februari

Kibatala: na uliwahoji wakiwa wanajitambua ni sahihi

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Uliongozwa kusema chochote kushuhudi majeraha ya kichwani

Shahidi: ee wakili aliniuliza waliumia wapi.

Kibatala: Uliongozwa kusema kuwa ulishuhudia wewe mwenyewe fulani aliumia kichwani uliongozwa au hukuongozwa?

Shahidi: Sikuongozwa

Kibatala: Uliongozwa kumhoji dereva kama yupo wa gari liliwapeleka Rahimu na Fikiri hospitali

Shahidi: Sikuongozwa

Kibatala: uliongozwa matibabu waliyopata Rahimu na Fikiri

Shahidi: Sikuongozwa

Kibatala: Raia wangapi walipigwa Risasi Mkwajuni

Shahidi: Sina kumbukumbu

Kibatala: mmoja au wiwili

Shahidi: sina kumbukumbu

Kibatala: unakumbuku juu ya Raia waliweka Polisi kwa zaidi ya siku tano mahabusu?

Shahidi: Sina kumbukumbu.

Kibatala: kuanzia tarehe 16 Februari ulikuwa unafanya kazi angalau mara mbili kwa Mkuu wa Polisi Mkoa Kinondo

Shahidi: nilisema nafanya kazi kwenye Ofisi za Mkuu wa Upelelezi wilaya

Kibatala: Umbali wa Mahabusi na Ofisi za upelelezi Wilaya

Shahidi: Ofisi na Upepelezi zipo kwenye jengo hilo hilo unapita mahabusu unapanda juu ghorofani ofisini kwangu

Kibatala: Ni sahihi kuwa washtakiwa kuhijiwa na wewe?

Shahidi: Mimi nilikuwa sehemu ya mahojiano hayo

Kibatala: hukuongozwa kusema chochote juu watuhumiwa walikana mashtaka yao hasa kuandamana?

Shahidi: sikuongozwa

Kibatala: Hukuongozwa kusema chochote juu ya washtakiwa wengine kusema hawakuwepo

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Ni sahihi washtakiwa watano hukuwatambua

Shahidi: Sikuwatambua kwa sababu sikuwaona kwenye maandamano

Kibatala: Uliongozwa kuzungumzia chochote kuhusu Ofisi ya Mkurugenzi

Shahidi: sikuongozwa

Kibatala: ushahidi wako ulisema kuwa waandamanaji walichochewa kwenda kwa Mkurugenzi?

Shahidi: ndio

Kibatala: uliongozwa kusema chochote juu ya kuwahoji Msimamizi wa uchaguzi au Ofisa wa uchaguzi

Shahidi: Sikuongozwa

Kibatala: Uchaguzi ni tukio la kisheria uliongozwa kutoa nyaraka yoyote uliyoonesha kuwepo kwa uchaguzi

Shahidi: Sikuongozwa.

Kibatala: Ulitoa nyaraka yoyote hapa mahakamani uliyokuwa ikonesha juu ya ufungaji wa kampeni?

Shahidi: sikutoa

Kibatala: tuzungumze kuhusu jeshi la Polisi nani analipenda jeshi la Polisi

Shahidi: Wananchi

Kibatala: kuwa na chuki na jeshi la Polisi ni kosa unatii sheria zote

Shahidi: inategemea kama umehamasishwa.

Kibatala: nataka tuchambue kusema nalichukia Polisi ni kosa mimi nikisema hapa nachukia polisi nikitoka nje nitakamatwa?

Shahidi: hukamatwi

Kibatala: kuchukia serikali ni kosa

Shahidi: ni kosa kutokana na kuhamasishwa

Kibatala: unajua watu waliohudhuria buibui hisia zao

Shahidi: sijui

Kibatala: unafahamu wale watu walihudhuria pale buibui wanaichukia serikali ama laa

Shahidi: sijafanya utafiti

Kibatala: Ni sahihi kwamba zamani unaweza kwenda jeshi la Polisi wakato wowote hakuna makamba makamba lakini siku hizi kuna mageti kuna askari na mabunduki mfano pale Osterbay nafahamu kuwa zamani jeshi la Polisi

Shahidi: ni sahihi kuna mabadiliko

Kibatala: Ni sahihi kuwa mwaka 2016 kuna kituo cha Polisi walishambuliwa askari wakafa wananchi wakashangilia mpaka mkuu wa jeshi la Polisi akatoa onyo kwa wananchi wanaoshangiliwa wakamatwe unakumbuka?

Shahidi: nakumbuka

Kibatala: unakumbuka kuna watu walikamatwa na wakashitakiwa?

Shahidi: nakumbuka

Kibatala: wananchi walishangiliwa kuuwa kwa Polisi kabla ya Buibui yaani tukio la 2016 ili kabla ya buibui

Shahidi: kimya

Kibatala: Tukio la wananchi kushangilia askari kuuawa ilikuwa kabla ya Buibui au baada

Shahidi: inategemea mtu mmoja akiandika mtandaoni sio wananchi wote

Kibatala: Tukio la IGP lilikuwa kabla au baada ya tukio la Buibui.
Baada ya kumaliza kuohjiwa na Wakili Kibatala, sasa ikiwa zamu ya Wakili Mwasipu

Mwasipu: Kuna mtu yoyote alikuja kulalamika kuwa meza yake imepinduliwa na mshtakiwa yoyote aliyekuwa mahakama

Shahidi: Hakuna

Mwasipu: kuna raia yoyote aliyekuja Ofisini kwako kulalamika juu ya kupata hofu kutokana na maandamano

Shahidi: walilalamika hawakuja Ofisini kwangu

Mwasipu: Shahidi kuna raia yoyote alikuja kuwa alifunga duka lake kutokana na hayo maandamano

Shahidi: Walilalamika

Mwasipu: Upelelezi umefanyika wapi

Shahidi: Kanda Maalumu ya Dar es Salaam

Mwasipu: Ni sahihi kwamba wewe ndiye uliyapanga askari aliyekuwa akiandika maelezo ya washtakiwa?

Shahidi: Ni mimi ndio niliyepeleleza

Mwasipu: Kwa mara ya kwanza ripoti yako uliipeleka kwa nani

Shahidi: kwa Mkuu wa Polisi Wilaya kisha .

Mwasipu: Computer ya aina gani

Shahidi: Disktop

Mwasipu: wakati zoezi la kuonesha huo mkanda wewe ulihusikaje

Shahidi: Nilikuwepo

Mwasipu: hizo sauti alizorekodi nani

Shahidi: kutoka kwa mwandishi wa muungwana

Mwasipu: huyo mwandishi wa muungwana alikuwepo?

Shahidi: hakuwepo.

Mwasipu: Uliwahi kusikia sababu washtakiwa kuandamana

Shahidi: nilivyowahoji walisema waliandamana kwenda ofisi ya mkurugenzi wa Kinondoni kwenda kuchukua barua za mawakala wao.

Mwasipu: kwa hiyo sababu ni barua ya utambulisho

Shahidi: ndio

Mwasipu: Kwa ufahamu wako watu wakiwa 20 wanakwenda ofisi ya mkurugenzi huku wanaimba au wanakunya maji wanakuwa wamefanya kosa au sio kosa?

Shahidi: inategemea na mazingira wanaweza kufanya kosa ua sio kosa

Mwasipu: kwa hiyo mazingira ya tarehe 16 uliyaona wewe kuwa yalokuwa kosa

Shahidi: yalikuwa kosa.

Mwasipu: Na sababu ya kwanza kwa kuwa walishika fimbo na maji

Shahidi: sio suala la kushika na mawe, walikuwa wengi wameshika mawe

Mwasipu: nilimuuliza hivyo

Hakimu:Swali lako linapendekeza majibu hayi

Mwasipu: nilimuuliza kwa kuwa walishika mawe walifanya kosa

Shahidi: walishika mawe na namna walivyokuwa ndio linakuwa kosa.

Mwasipu: kuna washtakiwa uliwatambua mahakamani hapa Mdee. Mbowe. Mashinji. Na Mnyika hawa uliiowatambua hapa nani alishika mawe na nani alishika fimbo

Shahidi: sikuwaona.

Mwasipu: shahidi umeleta mawe au fimbo hapa mahakamani kuonesha kwamba katika maandamano kulikuwa na mawe na fimbo

Shahidi: sikuleta kwa sababu

Mwasipu: sijauliza sababu, ni sahihi Pc Fikiri na Koplo Rahimu walidaiwa kupigwa na mawe

Shahidi: Sahihi

Mwasipu: hayo mawe umeyaleta

Shahidi: sikuyaleta

Mwasipu: umetamka hapa chanzo cha maandamano hayo ni hutuba zilizotolewa na washtakiwa ni sahihi?

Shahidi: sahihi.

Mwasipu: Wakati unaongozwa uliongozaa kutamka maneno yaliyopelekea watu kuandamana?

Shahidi: Sikutamka

Mwasipu: Shahidi umetoa maelezo yoyote yaliyotolewa na walalamikaji juu ya kuathirika na maandamano

Shahidi: yapo maofisa wa polisi..

Mwasipu: umeyatoa hujayatoa

Shahidi: sijayatoa

Mwasipu: shahidi ulisema umesikia kilele eneo la kawawa

Shahidi: sahihi

Mwasipu: hizo kelele ulijua nani anapiga

Shahidi: sikujua

Mwasipu: Shahidi kupiga kelele ni koda

Shahidi: sikusema mimi kama ni kosa.

Mwasipu: sikiliza swali langu

Shahidi:sio kosa

Wakili wa uteteza Prof. Safari naye akaendelea kumhoji

Profesa Safari : ulisema Akwelina aliketi kwenye daladala uliliona hilo

Shahidi: ndio

Profesa Safari : umeliona wapi

Shahidi: oysterbay

Profesa Safari : Ulisema gari ilitokea magomeni kuelekea Moroko risasi ilipiga upande gani wa daladala

Shahidi: nyuma

Profesa Safari : huyo mmiliki wa daladala muliandika maelezo yake

Shahidi: mimi sikuwa kwenye timu ya upelelezi .

Profesa Safari : dereva wa Dalala uliandika maelezo yake

Shahidi: kama nilivyosema sikuhusika

Profesa Safari : ni lazima Ofisa wa Polisi akiumia apelekwe Hospitali ya Barabara ya Kilwa ?

Shahidi: inategemea.

Profesa Safari : kuna ushahidi umetolewa OC Fikiri na Koplo Rahimu walilazwa wodi tofauti na wewe umesema wodi moja, ukweli ni upi?

Shahidi: wakati nawahoji walikuwa pamoja

Profesa Safari : ukiichukia serikali unakosa manufaa gani

Shahidi: unaweza kufanya vitendo vya uhalifu

Profesa Safari : hayo manufaa mimi nimeuliza manufaa

Shahidi: sijajua manufaa

Profesa Safari : ukiipenda serikali, unapata manufaa gani kuliko miye profesa niliye na wake wawili na benzi?

Shahidi hakujibu, shauri hilo litaendelea kesho tarehe 12 Septemba 2019.

error: Content is protected !!