Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Michezo Waziri Mkuu ataka wizara itoe taarifa kuahirishwa mchezo Simba na Yanga
MichezoTangulizi

Waziri Mkuu ataka wizara itoe taarifa kuahirishwa mchezo Simba na Yanga

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania
Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kutoa tamko kuhusiana na hatma ya mchezo kati ya Simba na Yanga uliotakiwa kuchezawa Jumamosi tarehe 8 Mei 2021 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Majaliwa ameyasema hayo leo tarehe 10 Mei 2021, Bungeni jijini Dodoma  Dodoma kwa kitaka Wizara kwa kushilikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuondoa hii sintofahamu iliyojitokeza.

Katika taaifa yake Majaliwa alisema kuwa jambo hili limevuta hisia za watanzania na hata nje ya nchi na hivyo kuagiza Wizara kutoa taarifa ya kuwa mchezo huo utachezwa lini pamoja na gharama za viingilio walizotoa watu kuingia Uwanjani.

“Timu hizi ndio ambazo zimebeba taswira za michezo hasa mpira wa miguu hapa Tanzania, kufuatia kero hii tayari nimeagiza Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoa taarifa haraka sana kwa watanzania, hasa mchezo wenyewe utachezwa lini na vile viingilo walivyotoa watanzania hatma yake ni nini.” Alisema Majaliwa

Aidha Wazili Mkuu aliwataka watanzania hasa wapenzi wa michezo ambao walitaka kuona mchezo huo kwa kulipa viingilio, kuipa muda Wizara kuja kutoa taarifa kwa kushilikiana na Tff.

“Niwasihi Watanzania na hasa wapenda michezo ambao pia walijiandaa kuona, kusikia lakini pia kutoa viingilio kwamba tuipe muda Wizara ije kutoa taarifa ikishilikiana na TFF ili watanzania wapate kujua hatma ya haya yote.” Alisema Waziri Mkuu

Mchezo huo namba 208 wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliahilishwa majira ya saa 12 jioni mara baada klabu ya Yanga kugomea mchezo huo kufuatia mabadiliko ya muda yaliyofanywa na Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) kutoka saa 11 muda wa awali hadi saa 1 usiku.

Katika taarifa Yanga waliyopitoa muda mchache mara baada ya kubadilishwa kwa muda iliwataka TFF pamoja na Bodi ya Ligi kufuata kanuni katika uwendeshaji wa mpira na kunuu kanuni ya 15(10) iliyosema kuwa mabadiliko yoyote ya muda wa kuanza kwa mchezo yatajulishwa ipasavyo kwa pande zote husika za mchezo angalau saa 24 kabla ya muda wa awali.

Mara baada ya sintofahamu hiyo jana TFF iliwaomba radhi watanzania na wapenda soka kwa ujumla na kuagiza bodi ya ligi kushughulikia haraka jambo hilo.

Mapema hii leo bodi ya ligi ilitoa taarifa yake ambao imepeleka jambo hilo kwenye kamati ya uwendeshaji na usimamizi wa Ligi (kamati ya saa 72) ambayo itakutana leo Tarehe 10 Mei 2021, kujadili mchezo huo mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wasimamizi wa mchezo huo wakiwemo Kamisaa na waamuzi.

 

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

error: Content is protected !!