Thursday , 18 April 2024
Home Kitengo Michezo Sakata Simba, Yanga lapelekwa Kamati ya saa 72
Michezo

Sakata Simba, Yanga lapelekwa Kamati ya saa 72

Spread the love

 

Kamati ua uwendeshaji na usimamizi wa Ligi (kamati ya saa 72) itakutana hii leo tarehe 10 Mei 2021, kwa ajenda moja ya kujadili kutofanyika kwa mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara kati ya Simba dhidi ya Yanga uliopaswa kuchezwa Jumamosi tarhe 8 Mei 2021. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo namba 208 uliahilishwa majira ya saa 12 jioni mara baada klabu ya Yanga kugomea mchezo huo kufuatia mabadiliko ya muda yaliyofanywa na Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) kutoka saa 11 muda wa awali hadi saa 1 usiku.

Taarifa kutoka ndani ya bodi ya ligi imeeleza kuwa imeshapokea taarifa kutoka kwa maafisa mbalimbali waliokuwa wasimamie mchezo huo ikiwemo kamisaa na waamuzi wa mchezo huo.

“Sekretariati ya bodi ya Ligi Kuu Tanzania tayari imepokea zote kuhusiana na mchezo tajwa hapo juu kutokana kwa maafisa mbalimbali waliopewa jukumu la kusimamia mchezo huo wakiwemo kamisaa na mwamuzi.”

“Hivyo basi kwa mazingatio ya kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom (kanuni:10 (2) na 10 (4) usimamizi wa Ligi kikao cha usimamizi na uwendeshaji wa Ligi maarufu kama kamati ya saa 72 itakutana Mei 10, 2021 pamoja na mambo mengine kujadili mchezo namba 208 kati ya Simba na Yanga uliopangwa kuchezwa Mei 8 2021.” ilieleza taarifa hiyo

Mpaka sasa hakuna sababu maalumu iliyoelezwa ya kusogezwa mbele kwa mchezo huo kutoka TFF na bodi ya Ligi.

Sababu za kuahilishwa kwa mchezo huo zilifuata mara baada ya Yanga kutoa tamko la kutokubaliana na mabadiliko ya muda huku wakinukuu kanuni ya 15(10) iliyoleza kuwa mabadiliko yoyote ya muda wa kuanza kwa mchezo yatajulishwa ipasavyo kwa pande zote husika za mchezo angalau saa 24 kabla ya muda wa awali.

Kwa kufanya hivi Yanga walibaki na msimamo wao na kuamua kupeleka timu Uwanjani majira ya saa 10 jioni huku wakiamini mchezo huo utachezwa saa 11 jioni na kuingia Uwanjani saa 11:10 na mara baada ya dakika 15 wakatoa timu uwanjani na kuondoka.

Dakika chache baadae kikosi cha Simba kiliwasili Uwanjani hapo na kupasha misuli moto majira ya saa 11:50 huku wakiamini mchezo huo utachezwa saa 1 usiku, dakika 10 mbele likatoka tangazo la kuahilishwa kwa mchezo huo.

Mara baada ya tukio hilo TFF iliwaomba radhi wadau na mashabiki wa waliojitokeza siku ya mchezo huo na kuahidi kushughulikia swala lao la viingilio.

Wakati bodi ya Ligi ikibainisha kukutana kwa kamati hiyo tayari klabu ya Simba imeshatoa tamko lake na kutaka Yanga kushushwa madaraja mawili na simba kunufaika kwa kupewa pointi kwa tafsili ya kuwa Yanga waligomea mchezo huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

error: Content is protected !!