July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zitto: Buhigwe msitishwe

Zitto Kabwe kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo

Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, amewataka wakazi wa Jimbo la Buhigwe, Kigoma wasitishike na watu wanaowashinikiza kuchagua mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika jimbo hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma…(endelea).

Amesema, kumekuwepo na baadhi ya watu, baada ya kuona upepo wa kisiasa unabadilika, wameanza kuwatisha wananchi kuwa wasichague upinzani kwa kuwa, hawataleta maendeleo.

Zitto ametoa kauli hiyo jana tarehe 9 Mei 2021, katika kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo wakati akimnadi mgombea wake Garula Kudra.

 “Kuna watu wanaowatisha na kuwalazimisha kutowapigia kura viongozi wa vyama vya upinzani, natambua hilo eti kwa madai hawezi kuleta maendeleo.

“Nataka niwambie, maendeleo hayaletwi na chama bali viongozi bora.

Mtu bora anaweza kupatikana kwenye chama hata kama ni kidogo,” amesema Zitto.

 Uchaguzi kwenye jimbo hilo, unatarajiwa kufanyika tarehe 16 Mei 2021, ni baada ya Dk Philip Mpango, aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

error: Content is protected !!