SERIKALI ya Tanzania imewataka waajiri wote nchini humo katika taasisi za umma kuhakikisha watumishi wanaoajiriwa kwenye taasisi zao wanapata mafunzo elekezi kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kabla ya kuanza kazi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Lengo ni kuhakikisha azma ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alitaka utumishi wa umma kuwa uliotukuka.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa jana Alhamisi, tarehe 18 Novemba 2021, wakati akizindua bodi ya ushauri ya chuo hicho.
Mchengerwa alisema, mafunzo watakayoyapata watumishi hao yatasaidia kuwajenga kimaadili, kutambua na kuiishi miiko ya utumishi wa umma, kujua mwelekeo wa Serikali, kuwa na mienendo sahihi inayotakiwa katika utumishi wa umma na kuwajengea uzalendo kwa taifa.
“Mafunzo haya ni muhimu sana kwa watumishi wa umma kuwajenga kiutendaji kwasababu leo hii ukipita kwenye taasisi za umma utabaini baadhi ya watumishi hawako hai kiutendaji kwa sababu ya kukosa mafunzo elekezi ambayo yangewajengea nidhamu ya utendaji kazi,’’ alisema Mchengerwa
Waziri huyo alisema, ukosefu wa mafunzo kwa watumishi wa umma yanasababisha baadhi ya watendaji na watumishi kutoelewana kwasababu binafsi hali inayofanya baadhi ya watendaji kutowapangia majukumu watumishi walio chini yao hivyo taifa linakosa mchango wao wakati Serikali inawalipa mshahara.
Katika kushughulikia masuala ya nidhamu ya watumishi wa umma, Mchengerwa aliwataka waajiri kuzingatia taratibu za kushughulikia masuala ya nidhamu ili kulinda haki za watumishi wa umma.
Awali, naibu waziri wa wizara hiyo, Deogratius Ndejembi ali sema Chuo cha Utumishi wa Umma kina jukumu kubwa la kuwajengea uwezo wa kiutendaji watumishi wa Umma na kuwaandaa wanaoingia kwenye Utumishi wa Umma ili wawe na mwenendo bora.
Alisema, chuo hicho hakitakiwi kushindana na vyuo vingine kwasababu hata wahiti
Nashukuru sana kwa taarifa nzuri.
Niwatakie maandalizi mema ya taarifa zijazo.
Rafiki yako,
Aliko Musa.