December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Pablo wa Simba kibaruani leo

Spread the love

KOCHA mpya wa klabu ya Simba Pablo Franco Martin, leo kwa mara ya kwanza atakiongoza kikosi cha Simba kwenye kibarua chake cha kwanza, dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mchezo huo ambao utapigwa kwenye dimba la Ccm Kirumba, Mwanza ambao utakuwa wa kwanza kwa kocha huyo toka alipokuja kuchukua mikoba ya Didier Gomes Da Rossa.

Akizungumza na waandishi wa Habari jana jijini Mwanza, Pablo alisema kuwa, anategemea kuibuka na matokeo kwenye mchezo huo, licha ya kukili kuwa Ruvu Shooting ni moja ya timu ngumu na wanacheza vizuri.

“Tutagemea kesho kupata mechi ngumu, hio timu inacheza mchezo mzuri na mgumu na tuliona walivyocheza na Yanga ni aina ya timu nzuri.” Alisema kocha huyo

Pablo anaiongoza timu hiyo ambayo ipo kwenye presha kwa sasa kutokana na matokeo waliyoyapa hivi karibuni, licha ya usajili mkubwa walioufanya kwenye dirisha la usajili mara baada ya kumalizika kwa Ligi msimu uliopita.

Aidha kocha huyoa aliongezea kuwa, kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huo na kupambania alama tatu ambazo zitawaweka vizuri kwenye mchezo wa Ligi.

 “Tupo tayari kwa ajili yamchezo wa kesho (leo) najua utakuwa mchezo mzuri  na tupo tayari kupambana na kupata pointi tatu.” Alisema kocha huyo

error: Content is protected !!