Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Visima 44 vyagundulika kuwa na gesi asilia
Habari Mchanganyiko

Visima 44 vyagundulika kuwa na gesi asilia

Spread the love

 

KATIKA kipindi cha miaka 60 ya Uhuru, Tanzania imefanikiwa kuchimba visima 96 vya mafuta na gesi ambapo visima 44 vimegundulika kuwa na gesi asilia. Anaripoti Selemani Msuya, Dar es Salaam … (endelea)

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mhandisi Charles Sangweni leo Ijumaa, tarehe 19 Novemba 2021, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa wizara na taasisi zake kuelezea miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania.

Mhandisi Sangweni amesema kuanzia mwaka 1960 kumekuwepo na juhudi za kutafuta mafuta na gesi asilia ambapo visima 96 vimechimbwa, 59 vikichimwa nchi kavu na 37 baharini.

Amesema katika visima 44 ambavyo vimegundulika kuwa na gesi asilia visima 16 ni nchi kavu na 28 ni baharini na kwamba juhudi za utafiti zinaendelea ili kupata vyanzi vingine.

Kaimu mkurugenzi huyo amesema hadi sasa wamefanya utafiti kwenye eneo la mraba 534,000 ambapo kilomita za mraba 394,000 ni nchi kavu na kilomita 140,000 ni baharini.

“Tunaadhimisha miata 60 tukiwa tumefanikiwa kuchimba visima 96 ambapo visima 44 vimegundulika kuwa na gesi asilia ambayo nyingine ndio inatumika kuzalisha nishati ya umeme kwa asilimia 60, PURA tunaendelea kuhamasisha wawekezaji katika eneo hilo ili waje kuwekeza na kutafuta vyanzo vingine,” amesema.

Sangweni ametaja maeneo yenye visima ni pamoja na Ruvu, Mkuranga Pwani, Ntorya, Mnazibay (Kijiji cha Msimbati mkoani Mtwara na SongoSongo mkoani Lindi.

Amesema uzalishaji ulianza mwaka 2004 kwa upande wa SongoSongo na mwaka 2006 kwa upande wa Mnazi Bay ambapo ambapo gesi iliyogunduliwa ni futi za ujazo trilioni 57.54, nchi kavu ikiwa futi za ujazo trilioni 10.06, baharini trilioni 47.48.

Mhandisi Sangweni amesema uamuzi wa Serikali kuanzisha PURA mwaka 2015 umeongeza kasi ya utafutaji wa mafuta na gesi na kuwataka wadau wote kwenye sekta hiyo kuwekeza katika eneo hilo muhimu kwa uchumi wa nchi.

Amesema hadi sasa Tanzania ina mikataba ya Utafutaji, Uendelezaji na Uzalishaji Mafuta na Gesi Asilia (PSA) 11, kati ya hiyo mitatu ipo katika hatua za uzalishaji na nane katika hatua mbalimbali.

Sangweni amesema pia kwa miaka ya hivi karibuni sekta hiyo imefanikiwa kushirikisha Watanzania kwa asilimia 90 kwenye kampuni zenye PSA.

“Ila jambo zuri zaidi kumeimarika kwa shughuli za ukaguzi wa gharam za matumizi katika mikataba ya PSA, ambapo hadi sasa tunatimiza miaka 60 kaguzi hizi zimewezesha kuokoa zaidi ya Sh bilioni 90,” amesema.

Amesema wamepitia changamoto mbalimbali lakini kwa kushirikiana na Serikali zimekuwa zikitatuliwa ambapo kwa sasa Tanzania inazalisha gesi asilia nyingi na mikakati yao ni kuongeza uzalishaji zaidi ili kushikiri kikamilifu kuifikisha nchi uchumi wa viwanda kufikia 2025.

Mhandisi Sangweni alisema mafanikio zaidi yatapatikana kupitia Mradi wa Usindikaji Gesi kuwa Kimiminika (LGN), ambapo fedha, ajira na viwanda vinavyotumia gesi kama malighafi vitaongeza uzalishaji.

1 Comment

  • Asante sana kwa habari nzuri.

    UWEKEZAJI MAJENGO ni blogu yenye maarifa ya jinsi ya kuwekeza kwenye ardhi na majengo na kufanikiwa. Ingia Google au bofya maandishi hayo juu.

    Rafiki yako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!