Wednesday , 27 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Waziri kivuli asema  Bodi ya Mikopo imevunja Katiba
Habari Mchanganyiko

Waziri kivuli asema  Bodi ya Mikopo imevunja Katiba

Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu
Spread the love

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Imetajwa kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika ibara yake ya 13-(2) inayokataza ubaguzi, anaandika Pendo Omary.

Uvunjifu wa Katiba unatokana na hatua ya HESLB Kutoa tamko kwa kile ilichokiita kuwa ni “sifa kumi za msingi”  kwa wale wanaotaka kuomba mkopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

Kati ya sifa zilizoanishwa na HESLB, sifa mbili kati ya kumi zimetajwa kuwa ni za kibaguzi, ambazo ni; waombaji ambao wazazi wao ni wakurugenzi au mameneja waandamizi katika makampuni binafsi yanayotambuliwa na mamlaka za mapato na usajili; Waombaji ambao wazazi wao ni viongozi wa umma au kisiasa ambao wanatajwa na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa umma.

Suzan Lymo, Waziri Kivuli Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni mbunge wa viti maalum(Chadema), amewaambia waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuwa “sifa hizo hazina uhalisia wa utekelezaji chanya kwa mazingira ya nchi yetu na ni kinyume na Katiba.”

Ibara ya 13-(2) ya Katiba inatamka wazi kuwa “Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka shart lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.”

Kifungu cha nne katika ibara hiyo hiyo kinasema ; Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamalaka yoyote inayotekeleza madaraka yakechini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya mamalaka ya nchi.

Mbali na uvunjifu wa Katiba, sifa hizo zimetajwa kuimarisha dhana ya ubaguzi na matabaka katika utoaji wa elimu ya juu nchini, wakati Tanzania tayari imetia saini mikataba ya kimataifa ambayo inalinda haki za binadamu, ikiwemo haki ya wananchi kupata elimu bila kubaguliwa.

“Miongoni mwa viongozi wa umma au siasa wanaotajwa na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni pamoja na madiwani wa kata na viti maalum. Kwa mujibu wa sheria za nchi yetu viongozi hao, pamoja na kuwa na majukumu makubwa yanayogusa maisha ya wananchi katika ngazi ya serikali za mitaa na kata, hawana mishahara, isipokuwa wanaishi kwa kutegemea posho ambayo haizidi Sh. 300,000 kwa mwezi…

“Pia, si kweli kuwa kila meneja na kila mkurugenzi kwenye kampuni iliyosajiliwa analipwa mshahara na kwamba si kila kampuni iliyosajiliwa ni kwa ajili ya kutengeneza faida kwani zipo kampuni zimesajiliwa na zinatambulika na malaka lakini ama hazifanyi kazi au zinafanya kazi za kujitolea klatika jamii hivyo wakurugenzi au mameneja wake nao wanajitegemea,” amesema Suzan.

Aidha, Suzan ameitaka serikali kutafuta mbadala au vyanzo vingine vya kugharamia elimu ya juu badala ya kuweka sifa zinazoendeleza ubaguzi.

Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wanufaika wa mikopo imekuwa ikishuka kutokana na ongezeko kubwa la wahitaji.

Mfano Chuo Kikuu cha Dodoma kwa mwaka 2015/2016 ilikuwa 23,786 hadi 16,758 kwa mwaka 2016/2017.Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanafunzi 1,105 kwa waliahirisha masomo mwaka 2016/2017 kutokana na sababu za kifedha wakiwemo wanafunzi 1082 wa mwaka wa kwanza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari Mchanganyiko

Wizara ya madini kurusha ndege ya utafiti wa madini Geita

Spread the loveKutokana na mchango wa wachimbaji wadogo wa madini kwenye pato...

Habari Mchanganyiko

Jafo aagiza kampuni za madini kuzingatia utunzaji mazingira, azitaka zijifunze kwa GGML

Spread the loveWAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia apewa tano ujenzi barabara Mtwara

Spread the loveWANANCHI wa Mkoa wa Mtwara, wameishukuru Serikali ya Rais Dk....

error: Content is protected !!