Wednesday , 27 September 2023
Home Kitengo Maisha Burudika Waziri Mwakyembe akemea ‘mshiko’ kwa watangazaji
Burudika

Waziri Mwakyembe akemea ‘mshiko’ kwa watangazaji

Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Spread the love

WAZIRI wa Habari, Utamaduni na Michezo,  Harrison Mwakyembe amekemea tabia ya baadhi ya waandishi wa habari kuchukua pesa (mshiko), ili wapige redioni nyimbo za wasanii, anaandika Hamis Mguta.
Amesema hatakubali tabia hiyo iendelee na kwamba vyombo vya habari vinatakiwa kulipa pesa ili vipige nyimbo za wasanii redioni na kuzionesha katika Luninga.

Mwakyembe ameyasema hayo leo katika ukumbi wa Vijana uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na Chama cha Wasanii wa Muziki wa Dansi Nchini (CHAMUDATA).

“Ni upendeleo tu, baadhi ya wasanii ndiyo wanasikika wengine wanazimwa kabisa haiwezekani kabisa wasanii wenyewe wanakufa wakiwa maskini na majina makubwa harafu kuna wengine wanabadilisha magari kila wiki,” amesema. 

Aidha amesema kuwa atahakikisha wasanii wananufaika na kazi zao na amewataka kuwa na mshikamano katika kupigania haki katika sanaa ya muziki ikiwemo kuwa na mikataba kati ya mmiliki wa bendi.

“Nimeelezwa kuwa kuna watu wengine hawataki mikataba, hapana ni lazima walazimishwe, twende kwenye ngazi tofauti kabisa ya mahusiano kwa sababu bila maandishi tunapoteza vitu vingi sana,” amesema.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Hassan Msumali amesema kutonufaika kwa kazi zao ni changamoto kubwa zinazowakumba huku wakiomba kupewa muda wa ziada kutokana na ukomo wa muda wa saa sita usiku waliowekewa.

“Upigaji wa nyimbo za dansi katika vyombo mbalimbali vya habari hautendi haki kwa mziki wa  dansi,” amesema.

Doreen Sinare, OAfisa Mtendaji Mkuu COSOTA amesema elimu inahitajika kwa wasanii kwa kuwa wengi wao hawajui utofauti kati ya hatimiliki na hakishiriki na kuwa changamoto kubwa katika muziki wa dansi zinatokana na kutokuwa na mikataba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Burudika

Mr. Eazi aachia Advice ikiwa ni ujio wa albam mpya

Spread the loveSTAA wa muziki kutoka nchini Nigeria, Mr.Eazi ni gwiji linapokuja suala...

Burudika

Stonebwoy adondosha ‘Dimension’ kolabo na Stormzy, Davido…

Spread the loveMSANII mahiri wa Afro- Dancehall kutoka nchini Ghana aliyesainiwa na...

Burudika

Mr Eazi, DJ Edu kuachia ngoma mpya ya Wena

Spread the loveBAADA ya kutangaza habari kubwa za ujio wa project ya...

Burudika

Makali ya Skillager kwenye ‘Busy Body’ usipime!

Spread the loveMWANAMUZIKI anayekuja kwa kasi kwenye game ya Afro Pop, Felix...

error: Content is protected !!