Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Wanafunzi elimu ya juu wapata mtetezi
Habari za Siasa

Wanafunzi elimu ya juu wapata mtetezi

Waziri Kivuli Wizara Ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Viti Maalum Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Suzan Lyimo
Spread the love

Waziri Kivuli Wizara Ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Viti Maalum Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Suzan Lyimo, amesema muongozo au masharti  ya kuomba mkopo uliotolewa na Bodi ya Mkopo wa Elimu ya Juu (HELSB), zinakasoro mbalimbali zinazowanyima Vijana wakitanzania uhuru wa kupata Elimu, anaandika Irene David.

“Elimu au kuelimika ni kibali cha maisha ya baadae kwa kuwa kesho ni kwa ajili ya wale walioiandaa leo,” sisi leo hatumwandalii huyu kijana elimu bora halafu umtegemee vipi kuijenga nchi yake kesho, amesema Lyimo.

Lyimo amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi zake zilizopo makao makuu ya Chadema amesema masharti hayo ni kama, Awe amemaliza kidato cha sita au awe na sifa linganish kama Diploma ndani ya miaka mitatu, waombaji ambao wazazi wao ni Wakurugenzi au Mameneja waandamizi hawatarajiwi kuomba na waombaji ambao wazazi wao ni viongozi wa umma au kisiasa ambao wanatajwa na sheria ya maadili ya viongozi wa umma.

Amebainisha kwamba katika sifa hizo zinazidi kuimarisha dhana ya ubaguzi na matabaka katika utoaji wa elimu nchini pia hazina uhalisia ya utekelezaji chanya kwa mazingira ya nchi na utekelezaji wake zipo kinyume na katiba.

Lyimo ameitaka serikali kutafuta njia mbadala au vyanzo vya kugharamia elimu ya juu mfano mabenki kwa riba nafuu na kuitaka tume ya Haki za Binadamu kuingilia kati suala hili .

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!