May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Aweso awafyeka vigogo wa maji

Juma Aweso, Waziri wa Maji

Spread the love

 

WAZIRI wa Maji nchini Tanzania, Jumaa Aweso, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa), Mhandisi Deusdedith Magoma. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea)

Taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano cha wizara hiyo jana Jumanne tarehe 16 Februari 2021, imesema, Waziri Aweso ameagiza Magoma kurejeshwa wizara ya maji “apangiwe majukumu mengine.”

Waziri Aweso, amemteua Mhandisi Ndele Mwansanga, kukaimu nafasi ya Magoma, wakati taratibu nyingine za kiutumishi za kumthibitisha kwenye nafasi hiyo zikiendelea.

Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Mwansanga, alikuwa mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya majisafi na usafiri wa mazingira jijini Mbeya (Mbeya Uwasa).

Kutokana na uteuzi huo wa Mhandisi Mwansanga, Waziri Aweso amemhamisha kituo cha kazi mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Iringa (Iruwasa), Gilbert Kayange kwenda kuchukua nafasi ya Mhandisi Mwansanga jijini Mbeya.

Katika kupanga vyema safu ya sekta ya maji, Waziri Aweso, ameagiza Bodi ya Ruwasa kutengua uteuzi wa meneja wa ujenzi wa Ruwasa makao makuu pamoja na meneja wa Ruwasa Mkoa wa Geita na “wapangiwe kazi nyingine ndani ya Ruwasa.”

Pia, Waziri Aweso, ameagiza bodi hiyo, kutengua uteuzi wa mameneja wa Ruwasa katika wilaya 20 za; Buhingwe, Uvinza, Mbulu, Musoma, Mbarali, Rungwe, Tandahimba, Nkasi, Kishapu, Baruadi, Songwe, Uyui, Misungwi, Magu, Bukoba, Babati, Igunga, Bunda, Ikungi na Newala na kutaka nafasi hizo zijazwe ndani ya wiki moja kwa kuteua watumishi walioonyesha bidii za kiutendaji.

error: Content is protected !!