WAZIRI wa Maji nchini Tanzania, Jumaa Aweso, amelazimika kutumia usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda ili kuweza kufika kwenye mradi wa maji wa Morong’anya uliopo jimbo la Morogoro Kusini Mashariki mkoani Morogoro. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Aweso akiwa na Mbunge wa jimbo hilo, Hamis Taletale, walitumia njia hiyo ya usafiri kutokana na eneo kilipo chanzo cha mradi huo kutofikaka kwa njia ya gari.
Mradi huo unaogharimu kiasi cha Sh 23.1 bilioni, pindi utakapo kamilika utahudumia wananchi zaidi 52,000 kwenye vijiji 19 vilivyopo katika kata 7 za Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki.
Mbali na kukagua mradi huo na kuridhika na maendeleo yake, Waziri huyo pia alishiriki zoezi la kupanda miti kwenye chanzo cha maji cha mto Mbezi utakaotumika kama chanzo cha maji kwa mradi huo mkubwa na wakihistoria katika jimbo la Morogoro Kusini Mashariki na Wilaya ya Morogoro
.
Pia ameshiriki kazi ya kuunganisha mabomba na kuyalaza ikiwa ni moja ya juhudi za utekelezaji wa mradi huu.
Leave a comment