Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Diwani Athuman ang’olewa Ikulu kabla ya kuapishwa
Habari za SiasaTangulizi

Diwani Athuman ang’olewa Ikulu kabla ya kuapishwa

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu Usalama wa Taifa, Diwani Athuman Msuya
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Kamishna Diwani Athumani, katika nafasi ya Katibu Mkuu Ikulu, na kumteua Mululi Majula Mahendeka, kushika wadhifa huo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Alhamisi, tarehe 5 Januari 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.

Rais Samia amemtumbua Kamishna Diwani, ikiwa zimepita siku mbili tangu amteua tarehe 3 Januari 2023. Awali, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

“Rais Samia ametengua uteuzi wa Kamishna Diwani, aliyemteua tarehe 3 Januari 2023. Aidha, Rais Samia amemteua Mululi Majula Mahendeka, kuwa Katibu Mkuu Ikulu. Mahendeka alikuwa Afisa Mwandamizi wa Ofisi ya Rais, Ikulu,” imesema taarifa ya Zuhura.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia atua Uturuki kwa ziara ya siku 5

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amewasili nchini Uturuki kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

error: Content is protected !!