Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wazee Chadema ‘wabisha hodi’ kwa Spika Ndugai, Rais Magufuli
Habari za SiasaTangulizi

Wazee Chadema ‘wabisha hodi’ kwa Spika Ndugai, Rais Magufuli

Spread the love

BARAZA la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wameeleza wasiwasi kuhusu gharama za matibabu ya Job Ndugai, Spika wa Bunge nchini India na mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kutokana na wasiwasi huo, wameitaka serikali kuwasilisha bungeni ripoti ya matibabu ya Spika Ndugai na mkataba wa SGR bungeni ili kupitiwa.

Wito huo umetolewa leo tarehe 5 Julai 2019 na Hashimu Juma, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Chadema wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

Juma ameeleza kuwa, baraza hilo lina wasiwasi kufuatia mradi wa SGR kutekelezwa pasipo kupitishwa na Bunge.

“Tunataka mikataba ya mradi wa Standard Gauge aliyosema Rais John Magufuli anatengeneza reli kutoka Dar es Salaam mpaka wapi sijui….,” amesema Juma.

Kuhusu ripoti ya matibabu ya Spika Ndugai, Juma amesema ni vyema serikali ikaiwasilisha bungeni ili kuueleza umma aina ya matibabu aliyopatiwa pamoja na ghama zake.

“Wakati serikali imeanza, Ndugai alikwenda kutibiwa India, matokeo yake aliporudi alisema katumia dola 12 milioni. Maradhi gani hayo, kafanya operesheni ngapi, kaenda hospitali gani?  hakuna, huo ni ufisadi.  Hiyo ilikuwa njia ya kuvusha kodi za Watanzania.

“Huo ni ufisadi wa kutisha, tunataka tuone ripoti zote zirudishwe, ziwasilishwe bungeni. Tunataka vyeti vya hoispitali, hesabu za madaktari na kafanya upasuaji ngapi,” amesema Juma.

Pia mwenyekiti huyo amesema, baraza hilo limeshauri serikali kuwafikisha katika Mahakama ya mafisadi, Spika Ndugai na wabunge wa CCM kwa madai ya kupitisha azimio la kutofanya kazi na Profesa Mussa Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Juma amesema, baraza hilo limetoa wito huo kutokana kwamba spika na wabunge hao wanakiuka katiba na sheria za nchi, kwa kukataa kufanya kazi na mtu anayesimamia hesabu za serikali.

“Kama kweli umedhamiria kufungua mahakama ya ufisadi, fisadi..  mchukue Spika Ndugai na wabunge wote wa CCM waliokataa kufanya kazi na CAG,” amesema Juma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!