Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NEC yapuliza kipenga jimboni kwa Tundu Lissu
Habari za Siasa

NEC yapuliza kipenga jimboni kwa Tundu Lissu

Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC)
Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeeleza kuwa, uchaguzi mdogo katika Jimbo la Singida Mashariki utafanyika tarehe 28 Julai 28 mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Jimbo hilo lipo wazi tangu tarehe 28 Juni 2019 baada ya Job Ndugai, Spika wa Bunge kumvua ubunge Tundu Lissu (Chadema) kwa madai ya utoro na kutojaza fomu za maadili.

Katika taaifa iliyotolewa na Jaji Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa NEC leo tarehe 5 Julai 2019 imeeleza kuwa, uchaguzi huo unafanyika baada ya Spika Ndugai kuzingatia matakwa ya kisheria katika kumvua ubunge Lissu.

Ameeleza kuwa, amezingatia matakwa ya kifungu cha 37 (1) (b) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi katika sura ya 343.

Kifungu hicho kinamtaka kutoa taarifa kwa umma kusuhusu kuwepo wa uchaguzi mdogo wa ubunge katika kwenye jimbo hilo.

Akizungumza taratibu kuelekea uchaguzi huo Jaji Kaijage amesema, kwa kuzingatia Katiba ya nchi na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kati ya tarehe 13-18 Julai 2019.

Na baada ya hapo amesea, uteuzi wa agombea utafanyika tarehe 18 Julai  2019 ambapo siku inayofuata, yaani tarehe 19-30 Julai 2019 kampeni zitakoma na tarehe 31 Julai 2019 uchaguzi utafanyika.

Kwenye taarifa yake hiyo, Jaji Kaijage amevikumbusha vyama vya siasa kuzingatia taratibu, sheria na kanuni za uchaguzi.

Wakati NEC ikitangaza uchaguzi huo, Lissu ambaye yupo Ubelgiji kwa matibabu baada ya kushambuliwa na risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma ameeleza dhamira yake ya kufungua kesi kupinga kuvuliwa ubunge wa jimbo hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!