Friday , 2 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Wawili wadakwa wakijifanya maofisa usalama, polisi
Habari Mchanganyiko

Wawili wadakwa wakijifanya maofisa usalama, polisi

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa
Spread the love

WATU wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam nchini Tanzania kwa tuhuma za kujifanya maofisa wa usalama wa Taifa, Polisi na Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA), kisha kutapeli Sh.35 milionil. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumamosi tarehe 12 Septemba 2020 na Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Kanda hiyo, wakati anazungumza na wanahabari jijini humo.

Kamanda Mambosasa amesema, mtuhumiwa wa kwanza ni Patrick Tarimo, aliyetapeli Sh.20 milioni kwa raia wa kigeni baada ya kujifanya Afisa Usalama wa Taifa.

“Mtuhumiwa huyo, mnamo tarehe 10 Agosti 2020 alitapeli kiasi hicho cha fedha kutoka kwa raia wa kigeni ambapo alimkamata na kujitambulisha yeye ni afisa usalama wa taifa na kufanikiwa kupata kiasi hicho cha fedha,” amesema Kamanda Mambosasa.

Mtuhumiwa wa pili ni, Castory Wambura, aliyejifanya Ofisa wa Polisi na TRA kisha kutapeli Sh.15 milioni wafanyabiashara watano wa Kariakoo.

“Mnamo tarehe 21 Agosti 2020 mtuhumiwa alitapeli kiasi hicho cha fedha kutoka kwa wafanyabiashara watano ambapo alijitambulisha yeye ni Ofisa wa Polisi na TRA,” amesema Kamanda Mambosasa.

Kamanda Mambosasa amesema, watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

Habari Mchanganyiko

Dk. Gwajima atoa maelekezo kwa maofisa maendeleo nchini

Spread the love  WAZIRI wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto,...

Habari Mchanganyiko

Kairuki awaweka mtegoni wakurugenzi watakaoshindwa kufikia malengo ya makusanyo

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na...

error: Content is protected !!