Tuesday , 30 May 2023
Home Habari Mchanganyiko Raia saba wa kigeni mbaroni tuhuma uhalifu mtandaoni
Habari Mchanganyiko

Raia saba wa kigeni mbaroni tuhuma uhalifu mtandaoni

SACP Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam
Spread the love

RAIA saba wa kigeni wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam nchini Tanzania kwa tuhuma za uhalifu kwa njia ya mtandao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Watuhumiwa hao ni, Adewale Nuren Oyedes, raia wa Nigeria. Ibrahim Darbey (Liberia), Cream Milton Elias (Liberia), Basube Dominic (DRC), Prince Tito (Liberia), Sibongile Arthur (Afrika Kusini) na Baljit Singh (India).

Akizungumza na wanahabari leo Jumamosi tarehe 12 Septemba 2020 jijini Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Jeshi la Polisi wa kanda hiyo amesema, watuhumiwa hao wamekamatwa nyakati tofauti, baada ya Polisi kufanya msako kati ya kipindi cha Agosti na Septemba 2020.

“Jeshi la Polisi katika maeneo mbalimbali ya Jiji, limefanya msako na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hawa ambao wamekuwa wakifanya utapeli na wizi kwa njia ya mtandao,” amesema Kamanda Mambosasa.

Kamanda huyo wa Polisi Dar es Salaam amesema, watuhumiwa hao baada ya kuhojiwa walikiri kujipatia fedha Sh.10 milioni kwa njia ya udanganyifu kupitia njia ya mtandao.

“Baada ya mahojiano walikiri kujipatia kiasi hicho cha fedha ambapo baadhi ya fedha hizo zilitumika kuanzisha duka la vinywaji vya pombe kali maeneo ya Tangi Bovu-Mbezi Beach, walinunua gari Toyota aina ya Mark X, televisheni mbili na magodoro,” amesema Kamanda Mambosasa.

Kamanda Mambosasa amesema, watuhumiwa hao saba watafikishwa mahakamani hivi karibuni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wenye ulemavu waiomba MISA-TAN iwajengee uwezo wa uhuru wa kujieleza

Spread the love  TAASISI ya vyombo vya Habari kusini mwa Afrika (MISA-TAN)...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wajawazito 2000 Korogwe washiriki Marathon, Mwenyekiti UWT amsifu Jokate

Spread the loveWANAWAKE wajawazito zaidi ya 2000 wilayani Korogwe mkoani Tanga wameshiriki...

Habari Mchanganyiko

Kirigini kuzikwa leo Butiama

Spread the love  MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini (1980-1985), Herman...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti

Spread the love  JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na...

error: Content is protected !!