Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Watu 17 wakamatwa uuzwaji jezi feki
Habari MchanganyikoMichezo

Watu 17 wakamatwa uuzwaji jezi feki

Spread the love

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limewakamata watu 17 kwa tuhuma za kuuza jezi feki za Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara klabu ya Yanga mara baada ya kufanyika kwa doria kali katika maeneo mbalimbali ya nchi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Kwa mujibu wa klabu ya Yanga, kampuni ya GSM ndio mwenye haki ya kutengeneza, kusambaza na kuuza jezi za klabu hiyo mara baada ya kuingia nao mkataba msimu wa 2019/20.

Taarifa ya jeshi la Polisi iliyotolewa na kamanda mkuu wa kanda ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro hii leo tarehe 2 Februari 2022, ilieleza kuwa zoezi la ukamataji wa jezhi hizo feki ulifanyika katika kipindi cha siku 27, kuanzia tarehe 2 Januari, 2022 mpaka tarehe 28 Februari 2022.

Katika zoezi hilo Polisi walifanikiwa kukamata jumla ya jezi 1208, katika maeneo yote waliofanya uchunguzi huo, huku Jijini Dar es Salaam, wakiwakamata watuhumiwa watano waliokutwa na jumla ya jezi 361.

Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam

Watuhumiwa hao ambao walikuwa ni Zahiri Hassan (17), aliyekutwa na Jezi feki 52, Majiba Ndahya (50) alikutwa na Jezi 124, Mohamed Ramadhani (26) alibambwa na Jezi 86, John Staslaus (19) alikamatwa na Jezi 39 na Emmanuel Kinasa (21) alinaswa na Jezi 60.

Aidha taarifa ya jeshi hilo iliendelea kueleza kuwa, mara baada ya kuwakamata watuhumiwa hao watano waliwataja wenzao kutoka visiwani Zanzibar, ambapo walikamatwa watuhumiwa watatu wakiwa na jumla ya jezi feki 36.

Jezi zingine 134, zilikamatwa kwa kushirikiana na polisi kutoka mikoa ya Tanga na Mwanza, ambapo waliwashikilia jumla ya watuhumiwa tisa waliokutwa ja jezi 811.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!