Saturday , 13 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Watoto watakiwa kujenga ujasiri dhidi ya unyanyasaji
Habari MchanganyikoTangulizi

Watoto watakiwa kujenga ujasiri dhidi ya unyanyasaji

Baadhi ya watoto waliofanyiwa ukatili
Spread the love

WATOTO nchini wametakiwa kujenga ujasiri kwa kupaza sauti pindi wanapoona kuna viashiria vya unyanyasaji na vitendo vya ukatili dhidi yao kutoka kwa baadhi ya wazazi, walezi na watu wengine ili kukomesha tabia hizo. Anaripoti Christina Haule … (endelea).

Ushauri huo umetolewa katika uzinduzi wa kampeni maalumu ya kutetea haki za watoto na vijana Manispaa ya Morogoro, na Mkurugenzi wa idara ya shule ya taasisi ya Pamoja Youth Organization (PAYO) ya jijini Dar es Salaam, Paul Gregory amesema kuwa watoto wanapaswa kuwa na ujasiri wa kufichua viashiria vya uvunjifu wa haki zao na vitendo vya ukatili kwao kila mara.

Gregory alisema, usiri na ukimya umekuwa ukitoa nafasi kwao kukandamizwa na kupelekea kuwarudisha nyuma kimasomo, kuathiri akili na msongo wa mawazo baada ya kutendewa matukio hayo.

Aidha amesema kuwa watoto wa kitanzania imefikia wakati waige mfano wa kitendo cha mtoto mwenzao, Anthony Petro (10) mkazi wa Ngara mkoani Bukoba aliyemzuia baba yake asiuze nyumba yao wanayoitegemea kwa kufichua jambo hilo kwa jeshi la polisi na kusaidia usitishaji wa uuzaji hivi karibuni.

“Anthony ni mwanafunzi wa darasa la kwanza kule Ngara, Kagera na ameweza kujenga ujasiri mkubwa kwa kumzuia baba yake asiuze nyumba baada ya kwenda kituo cha polisi na kutoa taarifa ya baba yake kutaka kuuza nyumba yao wanayoitegemea,” amesema Gregory.

Gregory amesema kuwa vitendo vingi vya uvunjifu wa haki za watoto hufanywa na watu wa karibu hivyo ni vyema watoto wenyewe kuanza kupasa sauti ili jamii isaidie ikishirikiana na vyombo vya sheria kama alivyofanya Anthony.

Naye Mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Pamoja ya Bonyokwa jijini Dar es Salaam, Mwasiti Hemes (10), amesema kuwa wana kila sababu ya watoto na vijana kuwa wajasiri hasa kwa kuwafichua watu wanaokandamiza haki zao na kuendesha vitendo vya ukatili dhidi yao.

“Ni matukio mengi wanafanyiwa watoto lakini watoto wengi wamekuwa wasiri sana hali inayopelekea matukio mengi ya ukatili, unyanyasaji na kukandamizwa kwa haki mbalimbali kutotambulika na jamii hata na vyombo vya sheria,” amesema Mwasiti.

Hivyo Mwasiti aliiomba Serikali kutumia nafasi hiyo kwa kuwakamata wakosaji wachache na kuwapeleka kwenye vyombo vya sheria kuwachukulia hatua kali ili iwe fundisho kwao na kwa watu wengine.

Akizungumzia unyanyasaji huo mkazi wa mtaa wa Area Six, kata ya Kichangani Manispaa ya Morogoro, Claudia Lucian amesema kuwa vitendo vya ukatili kwa watoto vimekuwa vikichangia kuporomoka kitaaluma shuleni.

Claudia alisema kuwa kuna matukio mbalimbali ya watoto kubakwa na hata ulawitiwa na watu wao wa karibu, huku wakikaa kimya na kwamba ifikie wakati wazazi tuwe na tabia ya kuelimisha watoto zetu na kuwaweka karibu ili waweze kusema kila linalowakuta kwa wakati.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Nchimbi aanika ugonjwa wa CCM

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emanuel Nchimbi,...

Habari za SiasaTangulizi

Makonda kuanika mawaziri wanaomtukana Samia

Spread the loveMKUU Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amewataka watu wanaowatuma mawakala...

Habari Mchanganyiko

Askofu ataka mafisadi, wauza mihadarati washughulikiwe kumuenzi Sokoine

Spread the love  MHASHAMU Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, Isaac...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mafuriko yaua 33 Morogoro, Pwani

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania imetoa tathmini ya athari ya mafuriko...

error: Content is protected !!