March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Simba, Yanga wakutanishwa mapema Kagame

Spread the love

MAHASIMU wa soka Tanzania, Simba na Yanga watakutanishwa mapema katika michuano ya Kombe la Kagame, linalotarajiwa kutimua vumbi nchini kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, ambapo Julai 5 watakutana katika mchezo wa mwisho wa Kundi C. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Kwa mujibu wa ratiba ya Cecafa iliyotolewa leo, inaonyesha Simba na Yanga zimepangwa Kundi C ikiwa ni mara ya kwanza katika miaka mitano iliyopita kwa wakongwe hao wa soka nchini kupangwa kundi moja katika mashindano hayo.

Akizungumzia kigezo kilichotumika kuipa nafasi Simba kushiriki kwenye mashindano hayo, Rais wa shirikisho la Soka Tanzania (TFF,) Wallace Karia amesema hiyo ni nafasi ya upendeleo baada ya Tanzania wenyeji wa mashindano hayo.

“Tuna nafasi ya timu tatu kushiriki kwenye mashindano hayo, kwanza Azam FC anashiriki kwa bingwa mtetezi, Yanga ni bingwa wa ligi kwa  msimu wa 2016/17”.

“Simba amepata nafasi ya ziada ya tatu kwa sababu tuna uwenyeji wa mashindano hayo na siyo vinginevyo,” amesema Karia.

Pamoja na Yanga na Simba kupangwa kundi mmoja bado wanafasi kubwa kwa wote kusonga mbele iwapo watashinda mechi zao mbili dhidi ya St. George (Ethiopia), Dakadaha (Somalia).

Makundi ya Kagame yamepangwa matatu na yatatoa timu mbili zitakazoongoza kwenye makundi hayo huku kukiwa na nafasi kwa timu mbili za upendeleo ‘best looses’ ili kupata timu nane zitazocheza robo fainali.

Makundi

Kundi A: JKU (Zanzibar), UGA (Uganda) , Azam (Tannzania)  na Kator FC (Sudan Kusini).

Kundi B: Rayon (Rwanda), Gor Mahia (Kenya), Lydia Ludic (Burundi) na Port (Djibout).

Kundi C: St. George (Ethiopia), Dakadaha (Somalia), Yanga na Simba za Tanzania.

error: Content is protected !!