Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wakuliwa watakiwa kulima pilipili kichaa
Habari Mchanganyiko

Wakuliwa watakiwa kulima pilipili kichaa

Zao la pilipili kichaa
Spread the love

WAKULIMA Mkoani Morogoro wametakiwa kuchangamkia fursa ya kilimo cha pilipili kichaa kutokana na zao hilo kuwa na soko huku likiwa na sifa ya kutoshambuliwa na magonjwa. Anaripoti Christina Haule … (endelea).

Hayo yalisemwa Mwekezaji kutoka Kampuni inayojishughulisha na mazao ya kilimo biashara (Vergrab Organic Farming Limited), Josephat Ligondo wakati akizungumza na vikundi mbalimbali vya wakulima vilivyopo katika Manispaa ya Morogoro.

Ligondo alisema kuwa wakulima wanaweza kubadilika kifikra na kuanza kulima zao la pilipili kichaa ambalo lilikuwa likilimwa zamani na mababu zetu ambapo wakulima wakizingatia kilimo chakena kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo wataweza kuona manufaa yake.

Akitolea mfano Ligondo alisema, mkulima anaweza kuotesha miche ya pilipili 12,000 kwa hekari moja na kupata mavuno baada ya kukausha kg 150 kwa wiki moja ambayo mkulima anaweza kuuza shilingi 4,500 kwa kilo na kuweza kupata kiasi cha zaidi ya shilingi mil 2.7 kwa mwezi.

Aidha alisema kuwa wakulima wa zao hilo sasa wataweza kunufaika kufuatia kuwepo kwa kampuni hiyo ya kununua zao la pilipili ambalo lina masoko makuu katika nchi za Malawi , Zimbabwe,Kenya na Uganda .

‘’sisi tukiingia mikataba na wakulima tunanunua kila wiki tani 8 hadi 10 sasa ni vizuri wakulima wachangamkie fursa hiyo ya soko’’alisema Ligondo.

Hata hivyo Mwekezaji huyo alisema zao la pilipili kichaa lina manufaa mengi ikiwemo kutumika kwa ajili ya kutengeneza chakula cha watoto, dawa aina ya volin na mabomu ya machozi.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa Evans manyanda alisema, kufuatia fursa hiyo ya soko la Pilipili iliyojitokeza Serikali ya mkoa itaangalia namna ya kujenga kituo maalumu cha kukaushia pilipili ili wakulima waweze kupelekea zao hilo kukausha na kuuza kwa urahisi baada ya kuingia mkataba maalumu na mwekezaji.

14 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!