Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Watanzania waliopo Israel watakiwa kujiandikisha kabla ya saa 6 usiku
Habari za SiasaTangulizi

Watanzania waliopo Israel watakiwa kujiandikisha kabla ya saa 6 usiku

Spread the love

KUFUATIA kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama nchini Israel na maeneo mengine ya jirani, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeandaa mpango wa kuwarejesha nchini Watanzania waliopo nchini humo na maeneo mengine ya karibu. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema Serikali imefikia uamuzi huo baada ya kufanya tathmini na kujiridhisha kwamba mazingira ya sasa yanaruhusu zoezi hilo kufanyika.

“Hivyo, Watanzania walio tayari kurejea nyumbani wanashauriwa kujiandikisha kwenye Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Tel Aviv, Israel kupitia barua pepe: telaviv@nje.go.tz au simu namba: +972 533 044 978 na +972 507 650 072, kabla ya tarehe 15 Oktoba 2023, saa 6 usiku,” imesema taarifa hiyo.

Hatua hiyo imejiri baada ya Wanamgambo wa Hamasi kutoka Ukanda wa Gaza – Palestina kuishambulia Israel ambayo imeendelea kujibu mapigo na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 2000.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!