Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Watanzania 2 wafa ajalini Zambia, wengine wajeruhiwa
Habari MchanganyikoTangulizi

Watanzania 2 wafa ajalini Zambia, wengine wajeruhiwa

Spread the love

RAIA wawili wa Tanzania, watatu wa Zambia na mmoja wa Kenya wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Serenje nchini Zambia, huku watu wengine 42 wakijeruhiwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana tarehe 27 Disemba 2023 na Afisa Mahusiano kwa Umma wa Jeshi la Polisi Zambia, Rae Hamoonga, ajali hiyo ilitokea juzi Jumanne, ikihusisha basi la abiria la Mkombe Luxury, lililokuwa linatokea jijini Johannesburg Afrika Kusini, kuja Dar es Salaam Tanzania kupitia Zambia, pamoja na lori la mizigo.

Ajali hiyo ilitokea mchana wa tarehe 26 Disemba 2023, baada ya basi la abiria kugongana uso kwa uso na lori la mizigo, lililokuwa linatokea Tanzania kwenda Zambia.

Hamoonga ametaja majina ya watu waliopoteza maisha kuwa ni, Davies Kolala (Mzambia), aliyekuwa dereva wa lori la mizigo, Rashid Athumani (Mtanzania), Chibala Abdnegal (Mzambia), Oscar Mwamulima (Mzambia), Ramadhan Abdallah (Mtanzania) na Eunice Jose (Mkenya).

Watoto nane ni miongoni mwa majeruhi 42  wa ajali hiyo, Watanzania waliojeruhiwa walikuwa 14, Wakenya nane, Wazambia 19 na mmo kutoka Uganda.

Taarifa ya Hamoonga imesema majeruhi wanaendelea kutibiwa katika hospitali nchini humo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

error: Content is protected !!