August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watakao kiuka taratibu uchaguzi CCM kufyekwa

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo

Spread the love

 

KATIBU mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM),Daniel Chongolo ametangaza kuwafyeka wagombea nafasi za uongozi ndani ya chama hicho endapo watakiuka misingi na utaratibu wa chama hususani kuanza kampeni mmapema na kujihusisha na vitendo vya rushwa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Chongolo ametoa taadhari hiyo leo Jumatano tarehe 13 Julai, 2022, akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wenyeviti wa ngazi ya matawi na mashina waliochaguliwa ndani ya chama hicho kwa Mkoa wa Dodoma.

Chongolo amesema kuwa wapo baadhi ya wanachama ambao kwa sasa wanaanza magenge ya kunyemelea nafasi mbalimbali zikiwemo za ubunge na nafasi nyingine ya juu jambo ambalo ni kinyume na utaratibu ndani ya chama.

“Ninataka kuwaambia wanachama wa chama cha Mapinduzi kuwa nitawachukulia hatua kali wanachama wote ambao wanaendeleza makundi ndani ya chama chetu na wengine upitapita kutafuta nafazi ndani ya chama.

“Lazima mkajua kuwa kwa sasa tunatambua kuwa viongozi waliopo ndiyo wanaotambulika lakini hatuna mbunge mwingine, diwani wala Rais tunajua muda wa kuanza kampeini bado.

“Mtu yoyote ambaye anatengeneza makundi kwa ajili ya kumchafua mtu mwingine kwakudhani anatengeneza njia ya kupata nafasi fulani tutamshughulikia kisawasawa na kwa bahati mbaya tunawajua na wanachokifanya tunakijua.

” Hatutasita kuwachukulia hatua kali hata kuwafuta uanachama kwani hatuna hasara nao wala faida nao. Kwa mtu wa aina hiyo hatavumiliwa na atachukuliwa hatua kwani chama chetu hakitaki makundi ya kuchafuana badala yake kinatakiwa kufanya kazi kwa kufuata misingi, taratibu, sheria na kanuni,” ameeleza Chongolo.

Katika hatua nyingine Chongolo ameweka jiwe la misingi katika jengo la kitega uchumi cha CCM lenye vyumba 172 ambapo hadi unakamilika mradi huo utagharimu kiasi cha Sh920 milioni na kuingiza Sh1.8 bilioni kwa mwaka baada ya kukamilika.

error: Content is protected !!