Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Watahiniwa 95,166 la 7 wafaulu mtihani elimu dini ya kiislamu
Habari Mchanganyiko

Watahiniwa 95,166 la 7 wafaulu mtihani elimu dini ya kiislamu

Spread the love

WATAHINIWA 95,166 kati ya 142,522, sawa na asilimia 66.7, waliofanya mtihani wa elimu ya dini ya kiislam wa darasa la saba, unaosimamiwa na taasisi ya Islamic Education Panel, wamefaulu mtihani huo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Matokeo hayo yametangazwa leo Jumatano, tarehe 12 Oktoba 2022 na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Taasisi za Kiislamu, Sheikh Mussa Kundecha, akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

Akitangaza matokeo ya mtihani huo uliofanyika tarehe 14 Septemba 2022, amesema wanafunzi 47,356 sawa na asilimia 33.23, kati ya watahiniwa hao waliofanya mtihani katika shule 3,710, ziliko kwenye halmashauri 151 za Tanzania Bara , wamepata ufaulu wa alama D na E.

Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Taasisi za Kiislamu, Sheikh Mussa Kundecha (katikati) akitangaza matokeo ya mtihani wa elimu ya dini ya kiislamu wa darasa la saba uliofanyika Septemba 14, 2022, katika shule za msingi 3,710.

Sheikh Kundecha amezitaja shule 10 zilizofanya vizuri katika mtihani huo, ambapo zimepangwa katika makundi mawili. Shule zilizomo kwenye kundi la shule zenye watahiniwa 20 au zaidi ni, Mumtaazi, kutoka jijini Mwanza. Istiqaama (Tabora), Rahma (Dodoma), Algebra Islamic (Dar es Salaam).

Dumila (Morogoro), Islamia (Mwanza), Hedaru (Kilimanjaro), Daarul Arqam (Dar es Salaam). Mbagala Islamic (Dar es Salaam) na Maarifa Islamic (Dar es Salaam).

Kwa upande wa shule zilizoko katika kundi lenye wanafunzi chini ya 20, Sheikh Kundecha amezitaja kuwa ni Galapo (Manyara), Sengerema Muslim (Mwanza), Nyakabanga (Kagera), Mhumbu Islamic (Shinyanga), Loliondo (Arusha). Nyarubale (Kagera), Rwanganilo (Kagera). Kamachumu Islamic (Kagera). Rera (Arusha) na Kiponzelo (Iringa).

Katika hatua nyingine, Sheikh Kundecha amezitaja shule zilizofanya vibaya  ikiwemo, Igonia (Singida), Mnganda (Singida), Kirongwe (Kilimanjaro), Ubilimbi (Shinyanga), Chankoko (Kilimanjaro), Ugaka (Tabora), Butobela (Geita) na Mferejini (Kilimanjaro).

Aidha, Sheikh Kundecha ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Elimu, iliingize somo hilo katika mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi, ili kuongeza idadi ya watahiniwa, pamoja na kuwajengea maadili mema watoto.

“Sasa hivi mnasema kuna changamoto ya kimaadili, wakati hamsimamii maadili ili yaelimishwe tangu mwanadamu mdogo sababu elimu ina mchango wake. Tunashauri Serikali ingefanya masomo ya dini kufanywa pamoja na mtihani wa darasa la saba, kama inavyofanywa katika kidato cha nne na sita,” amesema Sheikh Kundecha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!