Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Watafiti wa mbegu watakiwa kufuata kanuni
Habari Mchanganyiko

Watafiti wa mbegu watakiwa kufuata kanuni

Mbegu za mahindi
Spread the love

WATAFITI wa mbegu ndani na nje ya nchi wametakiwa kufuata sheria na kanuni zilizowekwa na Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) katika kutafiti mbegu mpya na kusajiliwa kwa wakati ili ziwafikie mapema wakulima katika msimu husika, anaandika Christina Haule.

Mkurugenzi Mkuu wa TOSCI, Patrick Ngwediagi amesema taasisi yake inavyofanya kazi ya utafiti wa mbegu kuanzia kwa watafiti wa mwanzo na kuzihakiki, kupitishwa, kuzisajili na baadae kuwafikia wakulima.

Ngwediagi amesema kwa mujibu wa sheria ya mbegu ya mwaka 2003 na marekebisho ya mwaka 2014 pamoja na kanuni za mbegu ya mwaka 2007 na marekebisho ya mwaka 2017 mtafiti anapogundua mbegu mpya anaifanyia utafiti kama inafaa na kisha anaipeleka kwenye taasisi hiyo.

Hivyo Ngwediagi alifafanua kuwa kufuatia kanuni na sheria hizo mtafiti wa awali wa mbegu anatakiwa kutumia muda wa miaka miwili kutafiti na ndipo mbegu hiyo ataifikisha TOSCI ambako itafanyiwa utafiti kwa kipindi cha msimu mmoja wa kilimo na kama inakubalika itaingizwa sokoni.

“Kimsingi TOSCI huwa tunapokea oda za majaribio kutoka kwa watafiti ambao ni wakulima ambao wamefuata sheria na kanuni zetu katika kutafiti mbegu na sisi kitaalamu kunazitafiti ndani ya msimu mmoja wa kilimo na baadae zinapitishwa, lakini kama zikikubalika,” amesema Ngwediagi.

Amesema utafiti huo huchukua muda wa mwaka mmoja TOSCI kufuatia matokeo ya majaribio ya utafiti wa aina mpya ya mbegu kupelekwa kwenye kamati ya taifa ya uidhinishwaji wa mbegu mpya ambayo huishauri kamati ya taifa ya mbegu   kwa ajili ya kutoa mapendekezo.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa watafiti wa umma na binafsi kufanya utafiti wa kutoa aina mpya ya mbegu ya alizeti ambapo inakidhi mahitaji ya watanzania kwani kwa sasa kuna upungufu mkubwa.

Kwa upande wake Mtafiti Msaidizi Idara ya Utafiti na Uendeshaji, Levini Msimbira kutoka taasisi hiyo aliwahamasisha watafiti kuogeza juhudi za utafiti na kupeleka maombi kwa mazao mbalimbali ili kuleta tija katika suala la kilimo na kuwafanya wakulima kuona manufaa ya kilimo.

Amesema kuwa katika utafiti wanaoufanya wameweza kupokea maombi mbalimbali ya utafiti wa mbegu za mazao na wao kuyafanyia kazi na kwamba kwa mwaka 2017 wana aina saba za mbegu za mahindi mapya, pia aina mbili za njugumawe, aina 10 za mahararage na aina tatu za karanga zipo kwenye majaribio.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!