August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli amwingiza Prof. Kitila serikalini

Prof. Kitila Mkumbo

Spread the love

RAIS John Magufuri amemteua Prof. Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na kuwa mpinzani wa kwanza kuingia serikali ya Awamu ya Tano, anaandika Hamisi Mguta.

Rais Magufuli alimteua Prof. Kitila mapema leo kuchukua nafasi ya Mhandisi Mbogo Futakamba aliyestaafu.

Prof. Kitila ambaye ni Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Da es Salaam na mwanzilishi wa Chama cha ACT Wazalendo amekubali nafasi hiyo na kujiuzuru naye yake ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho na kubaki mwanachama tu.

Baada ya uteuzi huo Prof. Kitila amemuandikia barua Kiongozi wa chama chake, Zitto Kabwe kuachia nafasi yake katika chama na kiongozi huyo amekubaliana na barua hiyo na kumtalia kila la kheri katika nafasi yake mpya.

Mhadhiri mwingine aliyeteuliwa katika uteuzi huo ni Dk. Ave Maria Semakafu kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia, awali alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS).

Wengine walioteuliwa na Rais Magufuli amemteua Dk. Leornald Akwilapo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Maimuna Tarishi aliyekuwa wizara hiyo amehamishiwa kuwa Katibu wa Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge).

Wateuliwa wote wataapishwa kesho katika viwanja vya Ikulu.

error: Content is protected !!