Monday , 4 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wataalaam wa miamba watua Hanang
Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the love

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali imepeleka wataalamu wa miamba ambao watatoa taarifa ya nini kilichotokea na nini kifanyike katika mlima wa Hanang ambao kutokana na maporomoko ya mlima huo, watu zaidi ya 47 wamefariki dunia na kusababisha majeruhi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)

Mhagama ametoa kauli hiyo leo Jumatatu baada ya kutembelea Kijiji cha Gendabi – Hanang akiwa ameambatana na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, pamoja na Wakuu wa Vyombo vya ulinzi na Usalama.

Viongozi hao wameongozwa na Mkuu wa Mkoa Manyara, Queen Sendiga wamefika katika Kijiji cha Gendabi ambalo ni  eneo lililoathirika na maporomoko ya matope kutoka Mlima wa Hanang yaliyotokea usiku wa kuamkia tarehe 3 Disemba 2023.

Akiwa eneo la tukio hilo, Mhagama, amewaomba wananchi hao kupokea pole ambazo zinatoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye aliagiza lazima kufika  eneo la tukio na kuona  nini kifanyike kwa dharura kuhusu uokoaji pamoja na makazi kwa waathirika hao.

“Mambo haya yakitokea  kuna mambo ya haraka  yanatakiwa yafanyike kwa dharura hivyo tumekuja na kushauriana namna ya kujipanga kwa pamoja ili kufanikisha jambo hilo kwa uharaka” ameongeza Mhagama.

Ameongeza kuwa, maelekezo ya Rais Samia kwanza kuona namna gani tunaweza kuendelea kuokoa watu na kazi hiyo wanaendelea nayo vikosi vya uokoaji, pia kuangalia namna gani ya kuweza kuwasitiri wenzetu waliotangulia mbele ya haki.

Kwa upande wake Bashungwa amesema kazi ya kufungua miundombinu ya barabara inaendelea ili kurahisia kazi za uokoaji na kufikisha huduma muhimu za kijamii katika meneo yaliyoathirika.

Amesema Wakala wa Barabara nchini ( TANROADS) tayari wamefungua barabara ya Singida-Babati ambayo awali ilikuwa haipitiki kutokana na kujaa tope na magogo ya miti kutoka milimani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwinyi aungana na Samia kuuaga mwili wa baba yake

Spread the loveRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mtoto wa Mzee Mwinyi amwaga machozi

Spread the loveMtoto wa Hayati mzee Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi ameshindwa...

Habari za SiasaTangulizi

Mzee mwinyi alikuwa mwanademokrasia wa kweli

Spread the loveMtoto wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Mwinyi alikuwa maktaba inayotembea

Spread the loveRais Samia Suluhu hassan amesema Hayati rais mstaafu, Ali Hassan...

error: Content is protected !!