Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Wanasayansi wagundua teknolojia ya kunyofoa VVU kutoka kwenye seli
AfyaTangulizi

Wanasayansi wagundua teknolojia ya kunyofoa VVU kutoka kwenye seli

Spread the love

TIMU ya wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Amsterdam cha nchini Uholanzi imesema imefanikiwa kuondoa Virusi Vya Ukimwi (VVU) kutoka kwa chembechembe seli zilizoambukizwa kwa kutumia teknolojia ya uhariri wa jeni ya Crispr iliyoshinda Tuzo ya Nobel. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Teknolojia hiyo ambayo inafanya kazi kama mkasi, ndani ya molekuli, hukata DNA zilizoathiriwa ili ziweze kuondolewa.

Matumaini hayo yanathibitisha kuwa wanasayansi hao wanaweza kuondoa virusi mwilini, ingawa kazi nyingi zaidi inahitajika ili kuangalia iwapo njia hiyo itakuwa salama na yenye ufanisi.

Dawa zilizopo za VVU zinaweza kuzuia virusi lakini sio kuviondoa.

Muhktasari wa matokeo ya teknolojia hiyo umewasilishwa na timu ya Chuo Kikuu cha Amsterdam kutoka Uholanzi katika mkutano wa matibabu wiki hii.

Timu hiyo imesisitiza kazi yao inabaki kuwa uthibitisho wa kinadharia na sio tiba ya VVU kwa sasa.

Naye Dk. James Dixon ambaye ni Profesa msaidizi wa teknolojia ya seli shina na tiba ya jeni katika Chuo Kikuu cha Nottingham nchini Uingereza ameunga mkono matokeoya teknolojia hiyi na kusema kuwa matokeo kamili bado yanahitaji kuchunguzwa.

“Kazi zaidi itahitajika ili kuonyesha matokeo chanya katika majaribio haya ya seli yanavyoweza kutokea katika mwili mzima kwa tiba ya siku zijazo,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!