Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Katimba awashika mkono Mama Lishe Mwandiga
Habari Mchanganyiko

Katimba awashika mkono Mama Lishe Mwandiga

Spread the love

Mbunge wa viti maalumu  Zainab Katimba amekabidhi mitungi ya gesi kwa vikundi vya  wanawake wajasiriamali katika kata ya Mwandiga halmashauri ya Kigoma mkoani Kigoma  ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluh Hassan katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia. Anaripoti Faki Ubwa… (endelea).

Akizungumza baada ya kukabidhi mitungi hiyo Katimba amempongeza Rais Samia kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini na kusisitiza kuwa hatua hiyo si tu itasadia kutunza mazingira lakini pia ni sehemu ya kuwahepusha wananchi na madhara yatokanayo na matumizi ya kuni na mkaa.

Mbunge huyo amewataka wanufaika wa mitungi hiyo kuwa mabolozi katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwenye maeneo yao ili dhamira ya  Rais Samia iweze kutimia.

”Binafsi nimekuwa nikigawa mitungi hii kwa wanawake na leo nimekabidhi mitungi hamsini ikiwa ni sehemu ya mitungi miambili ambayo nimegawa kiu yangu ni kuona jamii inaondokana na matumizi ya nishati ya mkaa na kuni kama ambavyo rais wetu amekuwa akihamasisha” alisema Katimba.

Baadhi ya wanufaika wa mitungi hiyo wamempongeza  Katimba kwa juhudi zake katika kuyakwamua makundi ya wanawake na kumtaja kama kiongozi mwanamke ambaye amekuwa begakwabega na wanawake wenzake mkoani humo.

Wanawake hao wamesema mitungi hiyo itawasaidia kufanya shughuli zao kwa urahisi na kuwawezesha watoto wao kusoma vizuri kwani hapo awali wamekuwa wakilazimika kuwatuma kutafuta kuni badala ya kwenda shuleni kuasoma.

” Hapo awali tumekuwa tukipata shida sana yaani mtu unatumia kuni hadi ule moshi unakufanya macho yawe mekundu ” alisema mmoja wawanufaika hao.

Katika hatua nyingine mbunge huyo amekabidhi mashuka katika kituo cha afya cha Mwandiga na zahanati ya Kiganza.

Katimba anaendelea na ziara yake inayolenga kuyafikia makundi mbalimbali ya wanawake mkoani Kigoma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

error: Content is protected !!