Monday , 30 January 2023
Home Kitengo Michezo Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi
Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love

 

UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) umewapongeza wanafunzi wanamichezo wa chuo hicho walioshiriki kwenye Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Vyuo Vya Elimu ya Juu Tanzania (SHIMIVUTA) kwa kutwaa kombe la ushindi wa kwanza kitaifa kwenye mchezo wa mpira wa kikapu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza kwenye hafla fupi ya kuwapongeza wanafunzi wanamichezo walioshiriki mashindano ya SHIMIVUTA yaliyomalizika hivi karibuni Jijini Mwanza, Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa kitaalamu Prof. Richard Kangalawe ameahidi kuendelea kuwawezesha wanafunzi kwa kuwapatia fursa ya kushiriki mashindano mbalimbali.

Prof. Kangalawe akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa chuo Prof. Shadrack Mwakalila alisema ushindi wa kwanza kitaifa kwenye mchezo wa kikapu ni kitu cha kujivunia na hii itaendelea kuhamasisha wachezaji kujituma zaidi katika mashindano mengine.

Aidha, aliitaja ushindi mwingine ulioletwa na wanamichezo hao kuwa ni pamoja na medali nane kwa wanariadha na michezo mbalimbali.

Kwa upande wake Naibu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala Dk. Evaristo Haule alisema pamoja na kwamba michezo ni afya lakini ushindi huu umekiheshimisha chuo na kukitangaza.

Aliwataka wanafunzi kutambua namna uongozi unavyowathamini na kuendelea kukua kwenye misingi mema ya maadili kwani ndiyo azma kuu ya chuo.

Hata hivyo, baadhi ya wanafunzi walioshiriki michezo walisema wamefarijika kwa namna chuo kilivyowathamini na kutambua mchango wao na kuahidi ushirikiano wa kutosha kwenye mashindano yajayo huku wakisisitiza wanawake kujitokeza zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

Michezo

GGML yaongeza udhamini kwa Geita Gold FC msimu wa 2022/2023

Spread the loveKAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imeongeza mkataba wa...

error: Content is protected !!