SERIKALI ya Marekani imetangaza kutuma vifaru 31 aina ya M1 Abrahams nchini Ukraine, vinavyoelezewa na maafisa wake kuwa bora zaidi duniani, vikiwa vinatosha kwa Serikali ya Ukraine kuunda kikosi kamili cha vifaru. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Uamuzi uliochukuliwa na Marekani jana tarehe 25 Januari 2023 umekuja baada ya wiki kadhaa za mazungumzo na washirika wake wakuu ikiwemo Ujerumani.
Ujerumani nayo jana imetangaza kuipatia Ukraine vifaru 14 aina ya Leopard 2 na kufungua njia kwa washirika wengine pia kutuma vifaru vilivyotengenezwa na Ujerumani.
“Wakati majira ya msimu wa baada ya baridi yanakaribia, jeshi la Ukraine linafanya kazi kulinda eneo wanaloshikilia na kujiandaa kufanya mashambulizi zaidi ili kuikomboa ardhi yao,” Rais Joe Biden alisema jana wakati akitangaza uamuzi wa kutuma vifaru nchini Ukraine zaidi ya miezi 11 baada ya wanajeshi wa kwanza wa Urusi kuingia Ukraine.
Rais Biden alisema Waukraine wanahitaji kuwa na uwezo wa kukabiliana na mbinu na mikakati ya Urusi inayobadilika kwenye uwanja wa vita katika muda wa karibu.
Leave a comment