Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6
Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Joseph Selasini (kulia) na James Mbatia
Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga kutoa uamuzi wa kesi iliyofunguliwa na wajumbe wa zamani wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha NCCR-Mageuzi, kupinga uteuzi wa wajumbe wapya, tarehe 6 Februari 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Tarehe hiyo imepangwa jana Jumatano na mahakama hiyo mbele ya Jaji Ephery Kisanya, baada ya mawakili wa pande zote mbili kuwasilisha hoja zao za kisheria dhidi ya mchakato uliotumika kuteua wajumbe hao.

Kesi hiyo Na. 570/2023 ilifunguliwa na wajumbe wanne wa zamani wa bodi hiyo wakiongozwa na Mohamed Tibanyendera, wakiiomba mahakama hiyo itamke wajumbe wapi halali, kwa madai kwamba kikao cha Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi kilichofanyika tarehe 21 Mei 2023, kilichotengua uteuzi wao hakikuwa halali kwa kuwa kiliitishwa kinyume cha sheria.

Akijitetea katika kesi hiyo, Tibanyendera ambaye kitaaluma ni Wakili Msomi, alidai kwamba kikao hicho kilikuwa batili kwa kuwa kiliitishwa kinyume cha Sheria kutokana na taratibu za kuitishwa kwake kutofuatwa.

Wakili Tibanyendera alidai kwamba, wao kama wajumbe wa bodi hiyo, hawakupewa wito wa kuhudhuria kikao kilichodai kuwaondoa katika nafasi zao, huku akidai kwamba kitendo hicho ni kinyume cha katiba ya NCCR-Mageuzi, inayotaka wito wa kushiriki utolewe siku 14 kabla ya kikao.

Katika hatua nyingine, Wakili Tibanyendera alidai kikao hicho kiliitishwa kinyume na taratibu na Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Martha Chiomba, bila kumshirikisha Mwenyekiti wake, Francis Mbatia.

Aidha, Wakili Tibanyendera alidai kikao hicho ni batili kwa kuwa kiliahirishwa hadi Septemba mwaka jana na kikao cha Kamati Kuu ya NCCR-Mageuzi, kilichofanyika Mei 2022.

Naye Wakili Hardson Mchau, alidai kwamba maamuzi ya kuondolewa wajumbe hao yalikuwa si halali na kwamba Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), ilithibitisha uteuzi wa wajumbe wapya bila kuthibitisha uhalali wa mabadiliko hayo.

Hata hivyo, mawakili wa wajibu maombi walikanusha madai hayo wakidai kwamba kikao kilikuwa halali na kilihudhuriwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, pamoja na maamuzi yake kuthibitishwa na RITA.

Katika kesi hiyo, Tibanyendera na wenzake wanamshtaki Makamu Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Joseph Selasini na wenzake pamoja na RITA na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kesi hiyo ni kesi ndogo ndani ya kesi kubwa Na. 150/2022, iliyofunguliwa na wanachama wa NCCR-Mgeuzi, kupinga kufukuzwa ndani ya chama hicho kinyume cha sheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

Habari za Siasa

Lissu: Miaka 30 ya vyama vingi haikupambwa kwa marumaru

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, Tundu...

error: Content is protected !!