Zaidi ya wanafunzi 130 wa shule ya msingi LEA na sekondari Kuriga waliokuwa wametekwa nyara na watu wenye silaha kaskazini magharibi mwa Nigeria mapema mwezi huu wameachiliwa jana Jumapili bila kujeruhiwa. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Utekaji nyara huo wa watu wengi huko Kuriga, katika jimbo la Kaduna ulitokea tarehe 7 Machi mwaka huu ikiwamo ni moja ya mashambulizi makubwa kwenye shule kwa miaka kadhaa na kusababisha mjadala nchi humo juu ya ukosefu wa usalama.
Jeshi lilisema kuwa mateka hao waliachiliwa mapema wakati wa operesheni ya ukoaji lakini halikutoa maelezo zaidi.
Msemaji wa jeshi la nchi hiyo, Jenerali Edward Buba alisambaza picha za watoto hao wakiwa wamevalia zare zenye vumbi ndani ya mabasi.
“Mateka waliookolewa ambao ni jumla ya 137 ni pamoja na wanawake 76 na wanaume 61. Waliokolewa katika jimbo la Zamfara na watafikishwa na kukabidhiwa kwa serikali ya jimbo la Kaduna kwa hatua zaidi,” alisema.
Walimu na wakazi awali walisema takriban wanafunzi 280 wenye umri wa kati ya miaka minane na 15 walitekwa nyara wakati wahalifu wenye silaha, wanaojulikana kama majambazi nchini Nigeria, walishambulia shule wakiwa kwenye pikipiki.
Leave a comment