Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wakwe kuingizwa katika bima ya afya kwa wote
Habari Mchanganyiko

Wakwe kuingizwa katika bima ya afya kwa wote

Spread the love

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu, amesema katika Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote, Serikali inapendekeza  wakwe kuingizwa katika bima hiyo.Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na wahariri pamoja na viongozi wa dini, jijini Dar es Salaam, leo Jumatatu, tarehe 23 Januari 2023, Serikali imeweka pendekezo hilo kutokana na ongezeko la uhitaji wa wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii kuwaunganisha wazazi au wakwe zao katika bima za afya.

Ummy amesema kuwa, bima ya kaya inachukua wategemezi sita, ikiwemo mke, mume, watoto na wazazi wa mwanachama.

“Wategemezi tuseme watakuwa sita, maana yake mchangiaji na mwenzake wake na watoto wanne, hatuwezi kuacha bima ikawa na watu 10 au 20, hivyo mwenyewe ataangalia katika watu sita kama utamuweka mama yako mzazi  au mkwe,” amesema Ummy.

Ummy amesema “tumeona watu wanawatoa watoto zao wanaingiza wazazi au wakwe sababu wanaumwa sana, anamtoa mtoto sababu haumwi sana anataka kumuingiza mzazi au mkwe. Tumeangalia tunavyoanza tunataka kuvutia watu.”

Waziri huyo wa afya amesema, katika muswada huo, Serikali inapendekeza bima ya kaya ya watu sita gharama yake iwe 340,000 kwa mwaka. Pia, inapendekeza kitita cha mafao ya msingi chenye gharama ya 66,000 ambapo wahusika watapa huduma za msingi za afya katika vituo vya afya, zahanati na hospitali za Serilkali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!