Sunday , 29 January 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Idadi watu China yapungua kwa mara ya kwanza tangu 1961
Kimataifa

Idadi watu China yapungua kwa mara ya kwanza tangu 1961

Spread the love

 

IDADI ya watu nchini China imepungua kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 60, huku kiwango cha uzazi nchini humo kikifikia rekodi ya chini – watoto 6.77 kwa kila wanawake 1,000. Vimeripoti vyombo vya habari vya kimataifa … (endelea)

Idadi ya watu mnamo mwaka 2022 ilikuwa bilioni 1.4118 na imepungua kwa 850,000 kutoka mwaka 2021.

Kiwango cha watoto wanaozaliwa nchini China kimekuwa kikipungua kwa miaka, na hivyo kusababisha sera nyingi kupunguza muelekeo huo.

Lakini miaka saba baada ya kutupilia mbali sera ya mtoto mmoja, imeingia kile afisa mmoja alichoeleza kuwa “zama za ongezeko hasi la idadi ya watu”.

Kiwango cha watoto kuzaliwa mnamo mwaka 2022 pia kilipungua kutoka 7.52 mnamo 2021, kwa mujibu wa Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya China, ambayo ilitoa takwimu hizo Jumanne.

Vifo pia vilizidi idadi ya waliozaliwa kwa mara ya kwanza mwaka jana – China iliingia katika kiwango cha juu zaidi cha vifo tangu mwaka 1976 – vifo 7.37 kwa kila watu 1,000, kutoka 7.18 mwaka uliopita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

DCI ajitosa uchunguzi matokeo uchaguzi mkuu Kenya

Spread the loveOFISI ya Mkurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Kimataifa

Uganda yaanza kuchimba mafuta

Spread the love  UCHIMBAJI wa kwanza wa mafuta kibiashara nchini Uganda umeanza...

Kimataifa

Afrika kusini waandamana kushinikiza serikali kumaliza tatizo la umeme

Spread the love  MAMIA ya wafuasi wa Chama cha upinzani nchini Afrika...

error: Content is protected !!