Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Majaji wanaotuhumiwa kwa rushwa Mbeya kitanzini
Habari Mchanganyiko

Majaji wanaotuhumiwa kwa rushwa Mbeya kitanzini

Spread the love

 

JAJI Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mustapha Siyani, ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Mbeya, ifanye uchunguzi dhidi ya tuhuma za baadhi ya majaji kupokea rushwa kwa njia ya miamala ya simu, zilizoibuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Rashid Chuachua. Anartipoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa jana tarehe 22 Januari 2023 na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Mahakama Kuu ya Tanzania, Artemony Vincent, muda mfupi baada ya Dk. Chuachua kutoa tuhuma hizo wakati akihutubia uzinduzi wa wiki ya sheria mkoani Mbeya.

“Kufuatia tuhuma hizi, Jaji Siyani, amemuagiza Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu-Kanda ya Mbeya, Rose Ebrahim kuwasilisha hoja hii kwa Uongozi wa TAKUKURU wa Mkoa huo kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya tuhuma hiyo ili kubaini ukweli.Ikithibitika pasipo na shaka kwamba tuhuma hizi zina ushahidi wa kutosha,” imesema taarifa ya Vincent na kuongeza:

“Na bila ya kuathiri hatua nyingine zitakazochukuliwa na vyombo husika, hatua za kinidhamu zitachululiwa kwa watumishi hao watakaothibitika kutenda kosa hilo. Ni matumaini ya uongozi wa Mahakama kuwa waliotoa tuhuma watakuwa tayari kuthibitisha ili sheriaichukue mkondo wake bila kumuonea mtu yeyote au kuchafua taswira ya Mhimili wa Mahakama na watumishi wake.”

1 Comment

  • Hivi mbeya kuna nini? Jamii taabu,kwenye kutoa haki-hakuna-haki,serikali wilaya inaweka mambo hivyo..& kwa wakulima shida

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Huawei Tanzania yatajwa miongoni mwa waajiri bora kimataifa

Spread the loveKAMPUNI ya Huawei Tanzania imetajwa kuwa mwajiri bora nchini na...

Habari Mchanganyiko

Waziri wa uchumi wa Finland atua nchini, kuteta na mawaziri 7

Spread the loveWAZIRI wa Masuala ya Uchumi wa Finland, Mika Tapani Lintilä...

Habari Mchanganyiko

Asimilia 79 wafeli somo la hesabu matokeo kidato cha nne

Spread the loveWATAHINIWA wa shule 415,844 sawa na asilimia 79.92 ya watahiniwa...

Habari Mchanganyiko

NECTA yafuta matokeo ya watahiniwa 333 kwa kuandika matusi, kudanganya, 286 yazuiwa

Spread the loveBARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta) leo Jumapili limetangaza kuyafuta...

error: Content is protected !!