Tuesday , 21 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wakulima wa korosho Lindi, Mtwara kuchanua na “Vuna Zaidi na NBC Shambani”
Habari Mchanganyiko

Wakulima wa korosho Lindi, Mtwara kuchanua na “Vuna Zaidi na NBC Shambani”

Spread the love

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua msimu wa pili wa kampeni yake  maalum kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi inayofahamika kama ‘ Vuna zaidi na NBC Shambani’ ikilenga  kuunga mkono na  kufanikisha lengo la serikali ya kuzalisha tani 700,000 za zao hilo kwa mwaka ifikapo mwaka 2025. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Dunstan Kyobya ameongoza hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika mkoani humo leo tarehe 29 Septemba, 2022 na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa zao hilo wakiwemo viongozi wa kiserikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS) na vyama vikuu vya ushirika maofisa wa benki wa Benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo wa NBC, Elibariki Masuke.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Dunstan Kyobya (wanne kushoto) akioneshwa moja ya simu janja (smart phone) na Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo wa benki ya NBC, Elibariki Masuke (wa tatu kulia) ikiwa ni sehemu ya zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwa washindi wa msimu wa pili wa kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani Mtwara leo. Wanaoshuhudia ni pamoja viongozi waandamizi wa benki ya NBC pamoja na wadau wengine wa zao korosho mkoani Mtwara.

Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Kyobya alisema imekuja wakati muafaka kwa kuwa inakwenda sambamba na mpango wa serikali wa kuhakikisha sekta ya kilimo inachangia pato la taifa kwa asilimio 10 ifikapo mwaka 2030.

“Na ndio sababu nawapongeza sana Benki ya NBC kwa mkakati huu ambao hapo tu kimasoko bali pia unaunga mkono jitihada za serikali kukuza sekta hii muhimu na pia inalenga kumkomboa mkulima. Wito wangu kwa wakulima wa korosho mkoa wa Mtwara na Lindi naomba sana tuwaunge mkono NBC kwenye hili,’’ alisisitiza.

Akizungumzia zawadi mbalimbali zinazotolewa kupitia kampeni hiyo ikiwemo trekta, maguta (Toyo), baiskeli, pikipiki, pampu za kupulizia dawa simu janja, kanga, mabegi na madaftari, Bw Kyobya alisema zinalenga kuunga mkono jitihada za mkulima katika kuboresha kilimo na uzalishaji hatua ambayo ina tija zaidi kiuchumi katika mkoa huo.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Dunstan Kyobya akizungumza na wadau mbalimbali wa zao la korosho mkoani Mtwara wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS), vyama vikuu vya ushirika mkoani humo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’

“Msisitizo wangu tu kwa wakulima ni suala zima la nidhamu ya fedha na kutumia vema mafunzo yanayotolewa na benki ya NBC kuhusu umuhimu wa kujiwekea akiba, matumizi ya bima mbalimbali ikiwemo bima ya afya pamoja na kuwekeza kwenye zana za kisasa za kilimo,’’ alisema.

Kwa upande wake, Masuke alisema msimu wa pili wa kampeni hiyo ya miezi mitatu  ni muendelezo wa mkakati wa benki hiyo wa kujidhatiti kwenye kuinua kilimo cha mazao ya kimkakati ikiwemo zao la Korosho kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara.

“Tunashukuru kuona kwamba kampeni yetu ya mwaka jana ilipokewa vizuri sana na wakulima wa korosho katika mikoa hii ya Lindi na Mtwara na zaidi tunajivunia kuona kwamba kampeni ile ilimalizika kwa mafanikio kwa wakulima ambapo tuliweza kukabidhi  kwa wakulima zaidi ya 150 ambapo tulikabidhi jumla ya pikipki 25, pampu za umwagiliaji zaidi ya 60, baiskeli 70, na trekta 1. Ni matumaini yetu mwaka huu mambo yatakuwa mazuri zaidi’’ alitaja.

 

Alisema katika kampeni ya mwaka huu wakulima hao pia watakuwa kwenye nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo baiskeli, pikipiki, pampu za kupulizia dawa na zawadi za kifamilia ikiwemo simu janja, kanga, mabegi na madaftari.’’

“Kwa upande wa wa vyama vya msingi (AMCOS) vinaweza kujishindia zawadi kubwa zaidi ikiwemo maguta (Toyo) pamoja na matrekta,ili walengwa hawa wote waweze kujishindia zawadi hizi wanatakiwa wafungue akaunti benki ya NBC na wapitishe fedha za malipo yao kwenye akaunti hizo na moja kwa moja watakuwa wameingia kwenye droo ya kujishindia zawadi hizi,’’ alifafanua

Wakizungumzia kampeni hiyo pamoja na mpango wa NBC Shambani kwa ujumla, viongozi wa AMCOS katika mkoa huo walisema umekuwa na tija kubwa kwa wakulima huku wakionesha kuvutiwa zaidi na suala la kutokuwepo kwa makato ya fedha zao pindi wanapopitisha fedha hizo kupitia akaunti zao za NBC Shambani.

“Pamoja na uwepo wa zawadi mbalimbali kwenye kampeni hii ambazo kimsingi zitavutia wakulima wengi kujiunga na benki ya NBC, pia tunavutiwa na kutokuwepo kwa makato ambayo yamekuwa yakituumiza hasa sisi viongozi wa AMCOS pindi tunapopitisha fedha za wanachama wetu kupitia akaunti zetu.

“Kupitia akaunti za NBC Shambani tunashukuru kuona kwamba changamoto hii imekwisha kabisa,’’ alisema Juma Hamadi Saidi  ambaye ni Katibu wa AMCOS ya Tandahimba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Geita, Mwanza waongoza kwa mbwa

Spread the loveNaibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yapata idhini kuwa wakala wa madalali wa DSE

Spread the loveBenki ya NMB imepata idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Waziri aipongeza NBS kwa mafanikio

Spread the loveNaibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande amepongeza Ofisi ya Taifa...

error: Content is protected !!